Je Unajua nini Kuhusu Kipindupindu?

Kipindupindu ni ugonjwa wa kuharisha na kutapika.Ugonjwa huu husababishwa navimelea vya bacteria, vimelea hivi huitwa kwa lugha ya kitaalamu “Vibrio cholerae”.

Vibrio cholerae

Dalili za Ugonjwa wa KIpindupindu.

Kuharisha mfululizo au mara kwa mara bila tumbo kuuma ambako kunaweza kuambatana na kutapika.

Kinyesi au matapishi huwa ya maji maji yasiyo na harufu, yanayofanana na maji yaliooshea mchele.

Kusikia kiu sana, macho kudidimia na ngozi kusinyaa.Hivi hutokana na upungufu wa maji mwilini.

Kuishiwa nguvu,kuhema haraka haraka na kulegea. Hali his hutokana na upungufu wa maji na madini mwilini.

Shirika la Afya la Dunia

Mwaka 2017,zaidi ya watu 4000 na vifo 90 vilitokana na kipindupindu Tanzania bara na Zanzibar.

Tanzania bara

Mwishoni mwa mwaka 2017,Wizara ya Afya ilihalalisha mpango wa kupambana na mlipuko wa kipindupindu.

Zanzibar

  • Toka mwezi wa 7 mwaka 2017,hakuna mgonjwa mpya wa kipindupindu aliyeripotiwa.

1 thought on “Je Unajua nini Kuhusu Kipindupindu?

  1. Asee kumbe Zanzibar wenzetu wamepiga hatua,,sasa daktarimkononi mnawasaidiaje watu wanaoishi kwenye maeneo yenye kipindupindu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center