Madhara hatarishi ya mafua na namna ya kujikinga

Mafua ni ugonjwa sugu sana katika jamii nyingi. Mara nyingi ugonjwa huu hausumbui sana watu na hupona wenyewe ndani ya wiki mbili, lakini yafuatayo yanaweza kuwa madhara hatarishi yanayoweza kuletwa na ugonjwa huu.

Mafua husababishwa na virusi na huuweka mwili katika hatari ya kushambuliwa na maradhi (bakteria) mengine na haya ndiyo maradhi yanayoweza kupelekea kupoteza maisha hasa kwa watoto na wazee.

-Madhara ya mafua

-Kukosa maji mwilini (dehydration)
-Kutapika na kuhara, ingawa hii hutokea zaidi kwa watoto kuliko watu wazima.
-Maambukizi ya mapafu (Maambukizi ya sikio)
– Maambukizi ya koo
– Maambukizi ya mifuko ya hewa puani (Sinusitis)

Pia mafua yanaweza kusababisha matatizo ya afya aliyonayo mtu kuwa magumu zaidi. Kwa mfano, watu wenye pumu wanaweza kupata mashambulizi ya pumu(asthmatic attacks) wakati wanaumwa mafua, na watu wenye matatizo ya moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure) hali yao huweza kuwa mbaya zaidi kwa sababu ya mafua.

Ifuatayo ni namna ya kujikinga wewe na wengine dhidi ya uginjwa huu

1. Epuka mawasiliano ya karibu.
Epuka kushikana na watu ambao ni wagonjwa. Unapokuwa mgonjwa, jiweke mbali na wengine ili uwazuie kupata ugonjwa hasa watoto.

2. Epuka kuwepo kwenye mikusanyiko.
Ikiwezekana usiende katika mikusanyiko isiyo ya lazima, kwa maana kuna hataru kubwa zaidi ya maambukizi katika maeneo hayo.

3. Funga kinywa chako na pua.
Funika kinywa chako na pua yako na tishu wakati wa kukohoa au kupiga chafya.

4. Safisha mikono yako.
Kuosha mikono yako mara nyingi, itasaidia kukulinda dhidi ya virusi vya mafua

5. Epuka kugusa macho yako, pua au kinywa (mdomo)
Mafua mara nyingi huenea wakati mtu anagusa kitu kilichoathiriwa na virusi na kisha hugusa macho, pua, au kinywa chake.

6. Fuata kanuni nyingine za kiafya.
Safisha sehemu zinazoguswa mara kwa mara nyumbani, kazini au shuleni hasa katika msimu wa mafua. Pata usingizi wa kutosha, fanya mazoezi, punguza msongo wa mawazo, kunywa maji mengi, na kula chakula chenye lishe, kunaweza kukusaidia kupona haraka zaidi.

Kwa wenye matatizo makubwa ya Mafua wanaweza pia kumuona daktari na kupata chanjo kila mwaka.