Maswali yanayoulizwa mara kwa mara juu ya Mafua

Maswali na Majibu!

Je, mafua yanaweza kupona kabisa ?

Inategemeana nini hasa ni chanzo cha mafua hayo. Kama imesababishwa na vijidudu kama bacteria, huweza pona pale mtu anapotumia dawa.

Kwanini wakati wa mvua watu wengi hupata mafua ?

Virusi vinavyosababishwa mafua hupenda mazingira ya unyevu nyevu na baridi. Hivyo hushamiri kipindi cha mvua. Hivyo basi watu wengi hupata mafua kipindi hiki.

Kwanini kila ninapokuwa kwenye mazingira ya vumbi, napata mafua makali ?

Mara nyingine mafua husababishwa na allergy ya vumbi, hii huambatana na makamasi mazito na kupiga chafya na pua kuwasha. Tiba thabiti ni kuepukana na mazingira hayo.

Nifanye nini nyumbani kwangu ili niepuke kupata mafua kila wakati ?

  • Futa vumbi na ishi mazingira safi
  • Usialale na ndoo za maji ambazo hazijafunikwa chumbani kwako
  • Vaa nguo za kukupa joto kipindi cha baridi na mvua
  • Usianike nguo mbichi/unyevunyevu chumbani kwako

Nifanyaje nipatapo mafua ili kusaidia kupona haraka ?

  • Pendelea kunywa maji mengi ya uvuguvugu
  • Kula machungwa kwa wingi au matunda mengine yenye vitamin C kwa wingi
  • Pata mda wa kupumzika Zaidi katika siku yako
  • Kama mafua yamezidi na homa inakuwa kali, nenda kituo cha afya kwa msaada Zaidi wa daktari.

Β