Sababu nne hatarishi za kupata Mafua

MAFUA

Sababu nne hatarishi za kupata Mafua

Utangulizi

Mafua ni nini?

Mafua ni ugonjwa wa kuambukiza unaopona wenyewe unaosababishwa na vijidudu mbali mbali aina ya virusi japo kirusi aina ya Rhinovirus ndio maarufu katika kusababisha

Huchukua siku mbili hadi tatu kabla dalili hazijaanza kuonekana Kwa lugha ya kitaalamu hujulikana kama upper respiratory infection ila kwa kizungu huitwa common cold.

Dalili za Mafua

  • Chafya za mara kwa mara
  • Makamasi kutoka puani
  • Pua kubana
  • Koo kuwasha
  • Sauti kukwaruza
  • Homa
  • Kuumwa kichwa
  • Kukosa hamu ya kula
  • Kujisikia uchovu

Sababu hatarishi

Majira ya mvua :ambazo husababisha watu kukaa karibu na hivyo kupelekea kusambaa kwa virusi kiurahisi zaidi

Watotoย 

Watu wenye kinga ndogo ya mwili:kama wagonjwa wa kisukari na wenye maambukizi ya ukimwi.

Mazingira yenye watu wengine:kwani unaweza pata virusi kirahisi