Kanuni za Utumiaji wa Matunda na Mbogamboga

KANUNI ZA UTUMIAJI WA MATUNDA NA MBOGAMBOGA

MATUNDA

  1. Matunda ambayo yapo katika uasili wake ni bora zaidi. Matunda na mboga zisizopikwa ni bora kuliko yale yaliyopikwa, ingawa kuna baadhi wanaopendelea na kuona kupika kidogo ni muhimu. Matunda yaliyowekwa kwenye container na kuhifadhiwa kwa muda, hasa yale ya madukani huwa na virutubisho vichache zaidi.

2. Hakikisha unaosha matunda vizuri kabla ya kula

3. Usile matikiti pamoja na vyakula vingine. Kula peke yake

4. Hakikisha unaloweka matunda makavu kabla ya kula

MBOGAMBOGA

  1. Tengeneza juisi ya mchanganyiko wa mbogamboga ambazo hazijakaa muda mrefu na hazijapikwa. Waweza kutumia kifaa cha kusagia (blender). Tumia kila siku angalau mara moja. Juisi hii ni bora ikitumiwa baada tu ya kutengeneza, ingawa waweza kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadae.

2. Pia, juisi nzuri yaweza kutengenezwa na mchanganyiko wa mananasi na mbogamboga. Hii huitwa “green drink”. Hutengenezwa pia kwa kutumia blender

3. Kwa baadhi ya watu, mfumo wa kumeng’enya chakula hauwezi kustahimili mlo wa mbogamboga mbichi. Kwa hawa, wasijilazimishe kutumia.

4. Kula kiasi cha kutosha cha mbogamboga mbichi, na sehemu kidogo ikiwa imepikwa. Njia nzuri ya kupika mbogamboga ni kurekodi kiasi cha maji kilichotumika na muda uliotumika kuvipika mpaka maji yote yalipoisha. Mfano, mboga ya “broccoli” huweza kupikwa kiasi kwa muda wa dakika 15 au kiasi zaidi kwa muda wa dakika 30. Kadiria kiasi cha maji kinachotumika kupika mboga hii kwa muda huu, na ubakishe kiasi kidogo cha maji baada ya kumaliza kupika

5. Usimwage maji yanayobaki kwenye sufuria baada ya kupika mboga! Fanya maji haya yawe sehemu ya mlo wako. Hivyo, pika kwa namna ambayo itaruhusu kiasi kidogo cha maji kubaki (si zaidi ya 1/8 ya kikombe) baada ya kupika. Kisha kunywa maji hayo pamoja na mlo wako. Mbali na maji hayo yaliyobaki baada ya kupika na glasi ya juisi fresh, usinywe kinywaji chochote pamoja na mlo.

6. Viazi ni vyakula vya pekee! Kata sehemu zenye vimacho vinavyoota, lakini usimenye. Sehemu ya ½ inchi ya nje ya kiazi ina madini ya kutosha ya “Potassium”, na madini haya ni muhimu mwilini!

7. Mbogamboga zote ni nzuri, lakini epuka kutumia spinachi kupita kiasi. Spinach ina kiwango kikubwa cha “oxalic acid” ambayo huweza kuathiri mifupa ya mwili kwa kuondoa madini ya “calcium”.

 

8. Mbogamboga zenye rangi ya kijani iliyokolea zina vitamini na madini kwa kiwango kikubwa zaidi.

 

9. Mbogamboga zenye nyuzinyuzi ni muhimu sana katika mlo, kwa ajili ya mishipa ya damu na sehemu za utumbo. Ni kinga dhidi ya magonjwa ya moyo na matatizo katika mfumo wa kumeng’enya wa mwili.

Je, ni kanuni ngapi kati ya hizi huwa unazingatia?

3 thoughts on “Kanuni za Utumiaji wa Matunda na Mbogamboga

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center