Je, unajua kuwa mama mjamzito anaweza kupata sonona(depression) kabla na baada ya kujifungua?

"Mmoja kati ya wakina mama 9 hupata sonona baada ya kujifungua"

Wakina mama wanahitaji malezi bora hasa kipindi cha ujauzito. Sonona wakati na baada ya kujifungua (ndani ya miezi 12) ni kitu ambacho wakina mama wengi hupitia bila kujua na kuathiri maisha yao ya kila siku.

Kila mtu huhisi huzuni wakati fulani lakini mara nyingi huzuni huu hupita baada ya siku chache, Sonona huleta huzuni ukaao kwa wiki zaidi ya mbili na hata miezi kadhaa.

Dalili za sonona wakati na baada ya uzazi ni zipi?

-Kulia mara kwa mara na kuwa na huzuni kila wakati.

-Kuwa na hasira kila wakati.

-Kufikiria kumdhuru mtoto na hivyo kuogopa kukaa na mtoto peke yako.

-Kujitenga na watu uwapendao na wale wakupendao.

-Kuhisi kama hutoweza kumjali mtoto.

-Kuhisi kama hana uhusiano mzuri wa mama na mtoto .

-Kujiona kama huna thamani na kama huna msaada wowote hasa kwa mtoto wako.

-Kukosa nguvu, kushindwa kukumbuka vitu au kufanya maamuzi.

-Kula sana au kukosa hamu ya kula kabisa.

-Kupata shida kulala au kulala sana.

-Kupata mawazo ya kujiua.

-Kupata maumivu hasa ya viungo yasiyosikia tiba.

Sio kila mtu atapata dalili nyingi, baadhi ya wakina mama hupata baadhi tu ya dalili hizi.

Β 

Nani yupo katika hatari ya kupata sonona baada ya uzazi?

-Wakina mama wenye historia ya kupata sonona baada ya kujifungua kama alishawahi kuzaa.

-Kuwa na historia ya sonona au magonjwa ya akili katika familia.

-Kutokea kwa shida wakati wa ujauzito mfano kifo cha mwanafamilia.

-Matumizi ya pombe au madawa ya kulevya.

-Kupata shida wakati wa kujifungua au mtoto kupata shida kiafya.

-Kukosa msaada kutoka kwa marafiki na familia.

depression2

nifanye nini nionapo dalili hizi?

Pindi uonapo dalili hizi, Zingatia yafuatayo:-

-Wahi hospitalini mapema na uwaone madaktari wa wanawake na wa saikolojia.

-Kula chakula bora.

-Fanya mazoezi.

-Tumia muda mwingi kupumzika.

-Pata msaada kutoka kwa familia, ndugu na marafiki.

KUMBUKA: Uendapo kwa daktari kumbuka kumtaarifu kama una ujauzito au unanyonyesha ili aweze kukupatia dawa ambazo hazitodhuru mtoto wako.

 

 
 

mambo muhimu ya kujua kuhusu sonona.

-Kama wewe ni mjamzito na unapata dalili hizi, Tambua kuwa ni kawaida, wakina mama tofauti hupata sonona.

-Mara tu upatapo dalili hizi ongea na daktari wako.

-Kitu cha mwisho na cha MUHIMU, kama kuna wakati unasikia sauti za watu au kuona vitu ambavyo watu wengine hawavioni au kutaka kujidhuru wewe au mtoto ni dalili zinazohitaji msaada wa haraka sana wa daktari.

"shukrani wakina mama wote kwa kazi kubwa mnayofanya"

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center