Vitamin C na mafua

Watu wengi wakipata dalili za mafua wanakimbilia vitamin c ikiwa ni kupitia juice, matunda au hata vidonge. Ni kirutubisho ambacho kwa mda mrefu watu wamedai husaidia kuponya mafua. Je ni kweli?

kifahamu kirutubisho hichi

Vitamin C ni nini?

Ni kirutubisho ambacho ni muhimu katika kuondoa uchafu mwilini (antioxidant) na hutumika katika ujenzi wa mifupa, misuli pamoja na mishipa ya damu. Pia inatumika katika utengenezaji wa protini iitwayo collagen na inasaidia mwili kufyonza iron.

Vitamin C inapatikana wapi?

Hichi kirutubisho kinapatikana kwa asili kwenye matunda (mf. machungwa, mapapai, mananasi, maembe n.k) na mboga mboga (mf. Nyanya, pilipili hoho, brocolli, cabbage, spinach n.k).Vile vile kuna "supplement" za vitamin c ambazo zinapatikana.

Vitamin C inaweza kutibu au kuzuia mafua?

Tafiti nyingi zimefanywa na majibu yamekuwa hayana uthabiti. Kwa ujumla imebainika kuwa vitamin c inaweza kusaidia kidogo au kutosaidia kabisa kuondoa dalili za mafua. Matumizi ya vitamin C baada ya kupata mafua hayasaidii kupunguza makali ya mafuta wala siku za kuugua mafua. Matumizi ya Vitamin c kila siku kabla ya kuugua mafua inaweza kupunguza mda ambao ugonjwa wa mafua utamsumbua mtuamiaji. Japo tafiti zinaonyesha ni kwa kiasi kidogo sana.

Vitamin C ni kirutubisho muhimu mwilini lakini hakina uwezo wa kuponya mafua japo inaweza kupunguza muda ambao mtu atasumbuliwa na ugonjwa huu iwapo alikuwa anapata kiasi cha kutosha cha vitamin hii kabla ya kuugua mafua.

Kiasi gani cha vitamin C kiahitajika kwa siku kiafya?

Kiafya manamke juu ya miaka 18 inapaswa apate miligramu 75 za vitamin C.
Mwanaume juu ya miaka 18 inapaswa apate miligramu 90 za vitamin C. Chungwa moja linakadiriwa kuwa na miligramu 70 za vitamin C. Hivyo machungwa mawili yanatosha kwa siku. Hitaji la vitamin C kwa watoto linatofautiana kulingana na umri kama inavyoonekana kwenye jedwari.
Kupata zaidi ya miligramu 2000 za vitamin c kwa mtu mwenye zaidi ya miaka 18 ni hatari kwani huweza sababisha kichefuchefu, kuharisha na hata mawe katika figo. Kiasi hichi hupungua umri unavyopungua kama inavyoonekana kwenye jedwari.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center