Miguu yangu inachanika(magaga) chanzo ni nini?? Part 1

Kupasuka visigino na sehemu zingine za unyayo wa miguu(magaga) limekua ni tatizo la kawaida kwa watu wa vijijini na huonekana sana kwa wazee na watoto

Watu wengi hua na tafsiri tofauti juu ya hili tatizo na wengine huwaza hili tatizo kua ni sehemu za maisha yao na hawawezi kuliepuka.

 

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kupasuka kwa ngozi za visigino(magaga) kama vile

  • Kuiweka miguu kwenuye maji kwa muda mrefu na badae kutopaka mafuta, hali hii huwakuta sana wakulima wanaolima sehemu zenye maji mengi au watu wanaofanya kazi za jeshi.
  • Ngozi kua kavu sana hivyo kushindwa kutanuka na kusinyaa kulingana na mahitaji ya mwili. Hali hii hupelekea kupasuka kwa ngozi endapo itahitajika kutanuka
  • Kua na uzito mkubwa, hii husababisha mgandamizo kwenye miguu kuwa mkubwa kwa sababu ya uzito mkubwa wa mwili hivyo husababisha kupasuka kwa ngozi ya visigino.
  • Upungufu wa virutubisho mwilini kama madini ya zinc, vitamini E pamoja na mafuta.
  • Kuvaa viatu ambavyo nyuma vipo wazi(open shoes, sandals) kwa muda mrefu, viatu vya aina hii hulazimisha miguu upande wa visigino itanuke zaidi.
  • Baadhi ya magonjwa kama vile kisukari, na magonjwa ya homoni(thyroid diseases).
  • Umri mkubwa.
  • Mtu kutozingatia usafi wa miguu yake.

tujiulize??

Je nini madhara ya kupasuka miguu(magaga)??

Je nifanye nini ili kuondoa tatizo hili??

 

Endelea kufuatilia posti zetu zijazo kwa majibu ya maswali haya na mengine mengi…

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center