Ni kwa nini nawashwa sehemu za siri?

Muwasho katika sehemu yoyote ile ya mwili humkosesha mtu uhuru, na uhuru huzidi jupotea pale anapowashwa sehemu za siri. Muwasho huu huweza kuwa kama mtu anaungua au kuhisi kuchomachoma . Sababu za mtu kuwashwa huhusisha sababu nyingi, pengine magonjwa au mabadiliko ya kimwili.

Tatizo la kuwashwa sehemu za hutokea zaidi kwa wanawake kuliko ilivyo kwa wanaume. Hii pia huchangiwa na maumbile ya sehemu hizo ambapo kwa wanawake iko wazi zaidi.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu za kuwashwa sehemu za siri;

  • Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama kisonono,haya hupelekea kuwashwa ikiambatana na dalili zingine nyingi.
  • Maambukizi ya fangasi;asilimia kubwa ya wanawake hupata maambukizi haya katika kipindi fulani cha maisha yao. Hasa pale kinga ya mwili inapokuwa chini au pale wanapokuwa wajawazito. Hii pia ni sababu ya kuwashwa na huambatana na kutoa uchafu mweupe na hata kuvimba kwa kuta za uke.
  • Kukoma kwa hedhi ,homoni ya estrogeni inaposhuka katika kipindi cha kukoma hedhi huleta mabadiliko katika uke na mara nyingi huwa pakavu na kuwasha pia. Hasa kwa wanawake wenye umri zaidi ya miaka 45.
  • Utumiaji wa vitu vyenye kemikali kwa sababu za usafi au urembo. Hii huhusisha matumizi ya sabuni, karatasi za chooni zenye manukato na kemikali na baadhi ya watu matumizi ya kondomu.
  • Maambukizi katika njia ya mkojo, hii pia husababisha kuwashwa kwani huwa vijidudu huendeleza maambukizi mpaka nje.
  • Aina za material ya nguo za ndani ,watu wengi wanaotumia nguo za pamba hawapati sana matatizo haya bali wanaotumia nguo za mipira na material nyingine hupata zaidi hali hizi.

Ukiwa nyumbani unaweza kufanya yafuatayo kama tiba au kinga ikiwa unawashwa sehemu za siri?

  • Tumia maji pekee kujisafisha ,epuka utumiaji wa sabuni kujisafisha.
  • Vaa nguo za material ya pamba kuliko material nyingine hii hurahisisha usafi na kuepusha maambukizi.
  • Jisafishe kutokea mbele kuelekea nyuma baada ya haja.
  • Jiepushe na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwa kuwa na ngono salama.

Ikiwa unakuwa na dalili hizi ni vyema ukamuona daktari kwa matibabu zaidi kwasababu sababu ya muwasho huo ni nyingi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center