Matangotango

matangotango ni nini?

Matangotango

ni ugonjwa wa ngozi ambao husababishwa na fangasi. Aina hii ya fangasi hupatikana kiasilia kwenye ngozi. Ikitokea fangasi hawa wakikua kupitiliza kiasi mtu hupata mabaka mabaka meusi au meupe kuliko rangi yake ya ngozi ( matangotango). Matangotango yanaweza tokea katika sehemu yoyote ya mwili ila sana sana hutokea kwenye mgongo, shingo, kufuani na mikononi.

sababisho

Sababu zinazochangia mtu kupata tangotango.
1. Kuwa na ngozi yenye mafuta sana 2.Hali ya hewa ya joto 3.Kushuka kwa kinga za mwili. 4. Mawazo (stress) 5. Kutoka jasho kwa wingi

maambukizi

Je matangotango huambukizwa kwa kugusana?
Ugonjwa huu hauambukizwi kwa kugusana kwa sababu fangasi anayeusababisha hukua asilia kwenye ngozi ya mtu.

tiba

Je matangotango yanatibika?
Ndio, matangotango yanatibika. Mtu mwenye matangotango anashauriwa kutumia shampoo zenye kemikali zinazoua fangasi, mfano (ketokonazole shampoo). Pia mtu huyu anaweza paka cream au lotion zinazotibu fangasi ili kupunguza ukuaji wa fangasi huyu kwenye ngozi yake.

kinga.

Nifanye nini ili kujikinga na matangotango?.
1. Usivae nguo za kubana sana. 2. Vaa nguo zinazoweza kufyonza jasho kama nguo za pamba(cotton). 3. Punguza mawazo (stress) 4. Kula vizuri na jali afya yako kiujumla. 5. Kama ngozi yako inamafuta usitumie vipodozi vyenye mafuta sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center