Je wajua jinsi ya kutumia mipira ya kike?

Mipira ya kike kwa jina lingine kondomu za kike

Mipira ya kike

 Mipira ya kike hutumika kama njia moja wapo ya uzazi wa mpango na kuzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

Mpira wa kike hutumika kama mubadala wa mpira wa kiume,ni mpira mwembamba ambao unatumika kuzuia mimba za bila matarajio na magonjwa mengine ya zinaa.

Inatumika na mwanamke

 

Mipira ya kike inafanyaje kazi?

Mipira ya kike inatengeneza kizuizi cha mbegu za kiume na majimaji mengine kupita kuingia mwilini, ikitumika kiusahihi huzuia mimba zisizotarajiwa na magonjwa ya zinaa.

Natumiaje?

Ni rahisi kutumia mipira ya kike japo kwa mara ya kwanza inaweza kuwa ngumu. Utakuta maelezo kwenye pakiti, lakini pia unaweza pata maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa afya ya mahusiano.

     Kwanza, angalia tarehe ya mwisho wa matumizi yaani ‘expiry date’

     Pili, Toa mpira kutoka kwenye pakiti kua muangalifu  usiipasue, usitumie meno au mkasi, na pia kua muangalifu na kucha ndefu au vitu vyenye ncha kali kama hereni ambavyo vinaweza kutoboa mpira huo.

     Tatu,chagua  namna ambayo itakuwa yenye urahisi kwako, kaa, chuchumaa, lala au simama katika namna itakayokufaa kuweza kuingiza mpira huo. Kisha ingiza upande uliozibwa kwenye uke hadi kiasi kirefu ambacho mpira huo unaweza ingia na mwisho itabaki sehemu a duara kubwa nje ya uke wako.

     Nne, wakati wa tendo hakikisha uume unaingia ndani ya mpira na sio pembeni, unaweza kumuelekeza mwenza wako kuingiza sehemu sahihi.

     Tano, baada ya tendo zungusha taratibu lile duara lililokuwa nje kisha vuta kiutaratibu kuzuia mbegu za kiume kumwagika.

     Sita, tumia mpira mpya kila ukitaka kushiriki tendo.

 

Kumbuka: Msitumie mipira wote wawili kwa wakati mmoja kwani huweza kusababisha misuguano na mwisho kupasuka wakati wa tendo la ndoa.

 

kushoto kondumu ya kike na ya kulia ni ya kiume

Mipira ya kike Vs mipira ya kiume

 

Mipira ya kike inafaida na hasara zake, zifuatazo ni nyanja mbalimbali juu ya faida za mipira hiyo ambayo itakuwezesha wewe kufanya maamuzi ya kutumia au la ;

     Umahiri. Umahiri wa mipira yote ya kike na ya kiume ni sawa endapo itatumika kwa usahihi wakati wote.

     Haina muingiliano . Kama ilivyo mipira ya kiume ambapo huvaliwa wakati wa tendo wakati uume umesimama na si kabla au baada ya hapo, lakini mipira ya mwanamke haijalishi muda huvaliwa hata masaa nane kabla ya tendo la ndoa hivyo husaidia kujiandaa mapema na kujinga zaidi hata kama mwenza wako( wa kiume) hatakuwa hana mpira wakati huo.

     Nyenzo Iliyotengenezewa. Mipira ya kiume (sio zote) hutengenezwa na nyenzo ziitwazo ‘latex’ wakati za kike hutengenezwa kwa kutumia nyenzo laini ziitwazo ‘nitrile’ japo sio zote, ambapo sio rahisi kusababisha mlipuko wowote wa vipele au miwasho baada ya matumizi. Vilevile mipira ya kiume ikitumika na kilainishi kama mafuta inaweza kusababisha kupasuka, wakati za kike zinaweza kutumika na kilainishi chochote bila kupasuka.

     Ukubwa wa mpira. Mipira ya kike ni mipana na mikubwa ambapo huleta nafasi kwa uume kupumua na humpa mwanaume nafasi ya kuweza kusimamisha uume kwa muda mrefu ata baada ya kufika kileleni (cumming).

Nifanye nini endapo mpira umepasuka wakati wa tendo?

 

 Mara chache mipira  ya kike hupasuka, Ila endapo imepasuka fanya yafuatayo;

     Toa uume mara moja

     Toa mbegu za kiume zote kadri ya uwezo wako.

     Epuka kusafisha ndani ya uke wako kwa kutumia vidole na sabuni nyingi maana huongeza hatari ya maambukizi zaidi.

     Kama hukuwa na njia nyingine yoyote ya uzazi wa mpango unaweza kutumia njia nyingine( dawa)  ambayo huzuia ujauzito ndani ya masaa 72 ‘emergency contraceptive’.

 Wataalamu wa kiafya hushauri kupima magonjwa yote yanayoweza kuenezwa kwa njia ya tendo la ndoa baada ya siku 10 baada ya tendo bila kinga au mpira kupasuka. kisha kurudia baada ya miezi mitatu kwasababu kila gonjwa linatofautiana katika wakati wake wa kuweza kugundulika.

Nifanye nini endapo mpira umepasuka na mwenza wangu ni muathirika wa vvu?

  Endapo imetokea kupasuka kwa mpira na unajua kuwa mwenza wako ni muathirika, wahi hospitali na upewe dawa ndani ya masaa 24 ya kuzuia maambukizi kisha uendelea na dozi ya dawa ya kuzuia maambukizi kadri utakavyoelekezwa na daktari.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center