Kikohozi kikavu na tiba asili

ย 

Kikohozi hutokana na aidha vijidudu ambavyo hushambulia njia ya hewa, aleji , michubuko katika njia ya hewa au magonjwa ya moyo.

Aina za vikohozi

Kuna kikohozi kikavu na kikohozi ambacho hutoa makohozi.

Kikohozi hasa kikavu kinaweza kuwa bugudha sana kwa mtu, hivyo kumsababishia maumivu ya kifua, kichwa na kushindwa kufanya kazi zake za kila siku.

ย 

Vifuatavyo ni vitu asilia vinavyopatikana majumbani vinavyoweza kulainisha kikohozi kikavu.

1. Asali.

Asali hulainisha koo na kupunguza kikohozi. Waweza weka asali kiasi kwenye maji ya vuguvugu au chai ukanywa

ย 

2. Tangawizi

Tangawizi hulainisha kikohozi kikavu na kupunguza muwasho kooni.

Waweza tafuna kipande kidogo au kunywa chai au maji yenye tangawizi.

3. Limao

Limao katika chai au maji ya moto pia husaidia kulainisha kikohozi kikavu

4. Maji ya moto yenye chumvi

Sukutua na kutema maji ya moto yenye chumvi ,haya husafisha koo, husaidia kupona kwa mikwaruzo ya kooni na kulainisha kikohozi kikavu.

5. Maziwa au chai ya moto.

Maji maji au vitu vya moto ni muhimu sana mtu akiwa na kikohozi kikavu. Hivi husaidia kuleta hali ya unyevu kooni hivyo kulainisha kikohozi.

6. Juisi ya vitunguu maji

Vitunguu maji husaidia kulainisha kikohozi kikavu na kukausha mikwaruzo ya koo

7. Vitunguu swaumu na binzari manjano.

Hivi hulainisha kikohozi kikavu. Waweza changanya vitunguu swaumu kwenye asali , binzari manjano kwenye maziwa.

ย 

Kifua kisipolainika ndani ya siku tatu basi fika kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi

4 thoughts on “Kikohozi kikavu na tiba asili

  1. Asante doctor kwa hii article!je kwa mtu mwenye kikohozi kikavu usiku TU wakati wa kulala,chanzo huwa ni nini?na nini kifanyike ili hii hali isijirudie?

  2. Asante doctor kwa hii article!je kwa mtu mwenye kikohozi kikavu usiku TU wakati wa kulala,chanzo huwa ni nini?na nini kifanyike ili hii hali isijirudie?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center