Kiuungulia ni nini?

Kiuungulia kwa jina liingine kwa kiingereza linaitwa heartburn


Kiuungulia ni hali ambao hutokea asidi kupanda kwenye  umio (esophagus) kutoka tumboni .Huleta maumivu ya kuungua ambao mhusika husikia  katikati ya kifua .Kiuungulia hutokea mara baada ya kula chakula, ila pia inaweza kumuasha mtu kutoka usingizini kwasababu ya maumivu ya kuungua .Watu wengine wanaweza pata kiuungulia  mara baada ya kula vyakula  au kunywa vinywaji fulani.

Hii hali inaweza kukaa kwa dakika kadhaa au masaa machache

Kiuungulia inatokea baada ya msuli wa kupeleka chakula kwenye tumbo hushindwa kufunga baada ya chakula hupelekwa tumboni na hivyo kupelekea asidi kurudi njia ambao haitakiwi ambao ni umio .

Dalili za kiuungulia

Dalili kuu ya kiuungulia ni maumivu ya kuungua katikati ya kifua pamoja na dalili ziingine

 • Ladha ya uchungu/tindikali kinywani
 • Kurudia kwa chakula kinywani
 • Hisia kama chakula kukwama kooni.
 • Maumivu kama ya kuungua kwenye kufua kinachotokea baada ya kula au hata usiku.
 • Maumivu yanayozidi wakati wa kulala au kuinama mara baada ya kula chakula.

Sababu hatarishi

 • Vyakula vyenye viungo vikali(spicy food) na
 • Bidhaa zenye citrus kama machungwa na
 • Vyakula vilivyokaangwa au vyenye mafuta na
 •  Chokoleti( choclate)
 • Kula kupita kiasi
 • Pombe
 • Vinywaji vyenye gesi(kama vile soda)
 • Kahawa
 • Uvutaji wa sigara
 • Uzito uliopitiliza (overweight)
 • Ujauzito

Jinsi ya kuzuia  kiuungulia kutokea

 • Kula mlo mdogo
 • Epuka kulala mara baada ya kula ila lala baada ya masaa mawili au matatu baada ya kula
 • Acha kuvuta sigara
 • Kuupunguza uzito
 • Kuupunguza ย mawazo
 • Epuka vyakula vinavyoleta kiuungulia kwako.
 • Epuka kuvaa nguo zinazobana
 • Epuka kula mlo uliopitiliza

9 thoughts on “Kiuungulia ni nini?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center