Sipati usingizi wa kutosha. Nifanyeje?

Kama unalo hili tatizo, Je, ni la muda gani? Hukutokea mara mojamoja au limekuwapo kwa wiki au miezi kadhaa?

Baadhi huamua kumeza vidonge vya usingizi ili kutatua tatizo hili. Lakini, je wafahamu athari zake?

Athari za Dawa za Usingizi

 • Wasiwasi
 • Huzuni
 • Kuwashwa ngozi
 • Kutotulia
 • Kupoteza hamu ya kula
 • Matatizo katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
 • Kutokuona vizuri
 • Kuchanganyikiwa
 • Kizunguzungu
 • Shinikizo la damu
 • Shida ya kupumua
 • Matatizo ya ubongo
 • Kupoteza kumbukumbu
 • Na kadhalika…

Wataalamu husema kuwa kama ukienda kulala muda muafaka, ukawa na hewa safi na ya kutosha chumbani na kupumzika katika ukimya, utapata kupumzika vya kutosha hata kama hupati usingizi kwa haraka kama unavyotarajia. Wengi wanaodai kutokupata usingizi wa kutosha usiku kiuhalisia hulala muda mrefu kidogo bila wao kujua.

Kuna wengine ambao hupata shida ya kupumua wakati wa kulala, ambapo mwili huacha kupumua kwa takribani dakika 2 wakiwa usingizini. Hivyo, hushtuka akiwa anahema kwa nguvu. Tatizo hili mara nyingi huambatana na shinikizo la damu, kiharusi na magonjwa ya moyo.

TIBA

 • Kukosa madini ya ‘Calcium’ na ‘Magnesium’ huweza kupelekea kuamka masaa machache baada ya kulala na kufanya ushindwe kupata usingizi tena
 • Kula mlo wenye lishe inayofaa. Fanya kifungua kinywa na chakula cha mchana kuwa milo yako mikuu. Kula mlo mwepesi wakati wa jioni na masaa angalau manne kabla ya kulala ili kuruhusu ubongo kupumzika unapolala badala ya kuhangaika kusimamia mmeng’enyo wa chakula
 • Vyakula vyenye kemikali za ‘amino acid’ huchochea usingizi mfano tende, matunda ya mtini na ngano
 • Epuka vyakula mfano jibini, chocolate, soseji, viazi (chipsi), sukarisukari, spinachi, nyanya na mafutamafuta hasa kabla ya kulala. Vyote hivi huwa na kemikali ya ‘tyramine’ ambayo huongeza utengenezaji wa kichochezi cha ubongo kiitwacho ‘epinephrine’
 • Fanya mazoezi ya kutosha na ya mara kwa mara wakati wa mchana au mapema jioni lakini si kabla ya kulala
 • Tembea nje kwenye hewa safi angalau kwa dakika 30-45 kabla ya kulala
 • Oga na maji ya moto kiasi saa moja au mbili kabla ya kulala
 • Baadhi hupendelea chumba kuwa kimya wakati wengine hupendelea kuwe na kelele kwa mbali. Ili kukidhi wote, waweza kuwasha feni
 • Mwamini Mungu. Huwapa pumziko la kutosha wale awapendao
 • Kuwa na ratiba maalum ya kulala na kuamka kila siku. Kuchelewa kulala huweza kupelekea tatizo la kukosa usingizi
 • Kama hupati usingizi, lala kitandani na pumzika. Hii hufaa sana kwa mwili, sawia na kulala usingizi kabisa
 • Chumba kisiwe cha joto sana kwa kuwa hupelekea kukosa hewa
 • Usitumie dawa za usingizi. Usitumie vilevi au dawa za kulevya. Usitumie vinywaji vya ‘caffeine’ mfano kahawa, hasa kabla ya kulala.

5 thoughts on “Sipati usingizi wa kutosha. Nifanyeje?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center