Zijue faida za tangawizi kwa afya

Mmea wa tangawizi husifika kwa faida zake ambazo hupatikana kwenye mizizi ya mmea huo. Huweza kutumika kama kiungo katika chakula au kama dawa ya asili. Huweza kuwekwa kwenye chai na kuongezewa asali. Hutumika kutengeneza pipi na mivinyo.

Mmea huu una matumizi mengi yenye faida kiafya. Matumizi hayo ni kama vile: • Huondoa sumu mwilini. • Huua vimelea mbali mbali vya magonjwa ndani na nje ya mwili. • Huondoa uvimbe mwilini na maumivu mbali mbali. • Hutibu saratani ya tezi dume, kansa ya kongosho, kansa zisababishazo choo kigumu, kansa ya mapafu, kansa ya damu nk. • Huzuia uzalishaji wa bakteria ambae husababisha vidonda vya tumbo. • Kuzuia kansa ya matiti, kutibu kansa ya kizazi na mirija ya uzazi. • Huongeza msukumo wa damu. • Husaidia kuzuia shambulio la moyo, kuzuia damu kuganda, kuyayusha kolesto, kusafisha damu. • Husaidia kuzuia na kutibu tatizo la kukakamaa kwa mishipa. • Hutibu shinikizo la juu la damu. • Husafisha utumbo mpana na kupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kunguruma. • Huondoa Gesi tumboni kirahisi zaidi. • Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. • Huondoa uchovu na kuzuia kutapika (kwa wale wanaosafiri barabarani kuondoa kichefuchefu).

• Huondoa maumivu yatokanayo na kukaa sehemu moja muda mrefu au kusimama, hutibu tatizo la miguu kuwaka moto. • Husaidia kuzalisha vimeng’enya mbalimbali ambavyo humeng’enya chakula. • Huzuia kuharisha. • Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu. • Hutibu homa ya kichwa. • Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi. • Hutibu homa za asubuhi azipatazo mama mjamzito. • Husaidia kupnguza homa ya baridi yabisi (inflammation of the arithritis). • Huimarisha afya ya figo. • Husaidia kupunguza uchovu utokanao na matibabu ya mionzi. • Ina madini ya potassium ambayo ni muhimu katika kuongeza mfumo wa kinga mwilini dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta z amoyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mkojo hupita. • Ita madini ya silicon ambayo huongeza afya ya ngozi, nywele, kucha na meno.

nitumie kiasi gani kwa siku.

Tangawizi hushauriwa kutumika chini ya gramu 4 kwa siku, zaidi ya haps huweza muleta kiungulia. pia husemekana kua na muingiliano na dawa za damu kama vile warfarin nk.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center