JE, UNAJUA UNAWEZA KUWA NA MIMBA YA UONGO ?

JE, UNAJUA UNAWEZA KUWA NA MIMBA YA UONGO?

Ndiyo, unafahamu kuwa inawezekana ukawa na mimba ya uongo wakati dalili zote za ujauzito unazipata ?. Ijue mimba ya uongo na dalili zake . . .

Mimba ya uongo inayofahamika kitaalamu kama Pseudocyesis ni muonekano wa dalili zote za ujauzito anazopata mwanamke wakati kiuhalisia hana ujauzito. Mwanamke anaweza kuwa na dalili zote za ujauzito kama kutapika mara kwa mara, shida ya kulala na hata kukosa hedhi lakini vipimo vikaonesha kutokuwepo kwa ujauzito. 

Tatizo hili ni tofauti na Mimba Zabibu ambapo urutubishaji wa seli za uzazi unatokea lakini badala ya mtoto kutungwa, inatokea nyama au uvimbe katika mji wa mimba.

Tatizo hili linasababishwa na mabadiliko ya homoni yasiyo ya kawaida yanayosababisha kutengenezwa kwa homoni zinazohusika na mabadiliko yanayotokea wakati wa ujauzito. Vinginevyo, tatizo hili linaweza kusababishwa na hali ya kisaikolojia tu.

Ili tatizo hili litambulike kitaalamu kama mimba ya uongo ni lazima mwanamke husika aamini kabisa kuwa ana ujauzito kutokana na dalili zake na sio kuigiza. Wanawake wengine huweza kupata dalili za juu kabisa kama kutanuka tumbo au hata kusikia kijusi kikicheza tumboni. 

Cha kushangaza zaidi,  dalili hizi zinaweza kumpata hata mwanaume ambaye mwenza wake ana ujauzito. Katika tatizo hili linaloitwa Cauvade Syndrome, mwanaume kwa kumuonea huruma mwenzie anaweza kufikia hata kupata uchungu wa mimba.

Kwa upande mwingine, hakuna tiba maalumu ya tatizo hili kwani hakuna chanzo halisi cha ugonjwa. Pamoja na hilo, mgonjwa anaweza kusaidiwa kuondoa dalili anazozipata kama kukosa hedhi au kutanuka tumbo baada ya kuthibitishwa kwa vipimo kama ultrasound kwamba hana ujauzito. Pia, unashauriwa kumuona mtaalamu wa tiba ya saikolojia kupata msaada zaidi.

2 thoughts on “JE, UNAJUA UNAWEZA KUWA NA MIMBA YA UONGO ?

  1. Hello Vinnie !, asante kwa swali lako zuri. Molar pregnancy inayojulikana kama Mimba Zabibu kwa kiswahili ni tofauti na Mimba ya Uongo (Pseudocyesis) kama ifuatavyo;

   – Mimba ya uongo hutokea pale ambapo hakuna kijusi (fetus) kilichotengenzwa wala uvimbe wowote kwenye mji wa mimba (uterus) na huthibitishwa kwa mbinu za kitaswira kama ultrasound. Hii husababishwa tu na mabadiliko ya homoni au matatizo ya kisaikolojia kwa mfano mwanamke anayetamani sana kupata mtoto.

   -Mimba Zabibu (Molar Pregnancy) hutokea baada ya urutubishaji kufanyika na badala ya kijusi kutengenezwa, inatengenezwa nyama tu (abnormal mass without form). Hii husababishwa hasa kutokana na matatizo ya vinasaba (genetic).

   Unaweza kubofya neno Mimba Zabibu lenye rangi ya blu hapo juu na utapelekwa moja kwa moja kwenye chapisho letu tulipoelezea kwa kina Mimba Zabibu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center