faida za mazoezi kwa afya ya uzazi

"kinga ni bora kuliko tiba"

Kuna msemo unasema “kinga ni bora kuliko tiba” …hii ina maana kwamba kuliko kusubiri mpaka upate madhara au magonjwa ndipo utafute tiba ni bora zaidi  kufanya mambo yatakayo kupunguzia au kukuondolea kabisa hatari ya kupata matatizo hayo.

 

mazoezi naafya ya uzazi

Kwa upande wa afya ya uzazi moja kati ya kitu muhimu sana ni pamoja na mazoezi ya mwili na viungo vyake. Tafiti  nyingi zimeripoti faida nyingi sana za mazoezi ya mwili na viungo katika kupunguza  au kuondoa kabisa matatizo ya afya ya uzazi.

Faida za mazoezi kwa afya ya uzazi ni pamoja na;

1;Mazoezi yanapunguza hatari ya  kupata matatizo ya kusimamisha kwa wanaume. Tafiti mbalimbali za kitaalamu zinaonesha kuwa mazoezi yanasaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia magonjwa ya moyo na pia uimara wa mishipa ya damu ya uume hivyo mzunguko wa damu mzuri katika eneo hilo. Tafiti pia zinaonesha ya kua baadhi ya watu wenye matatizo haya hupotea baada ya kuanza kufanya mazoezi.

2;Mazoezi hupunguza hatari ya kupata dalili za tezi dume. Mtu anaefanya  mazoezi hupunguza hatari ya kupata dalili za tezi dume kwa zaidi ya nusu ukilinganisha na mtu asiyefanya mazoezi.

3;Mazoezi huimarisha ubora na kiwango cha mbegu za kiume. Tafiti zinaonesha ya kua mtu anayefanya mazoezi huzalisha kiwango kingi cha mbegu za kiume na bora ukilinganisha na mtu ambaye anaaka tuu bila kazi au mazoezi ya kumtoa jasho kwa zaidi ya masaa 20 kwa siku.

4;Mazoezi humfanya mtu kuwa mwenye nguvu na mwenye pumzi ya kutosha hivyo kushiriki tendo la ndoa kukamilifu bila kumkwaza mweza wake.
5;Mazoezi hupunguza uzito, mafuta ya mwili, kiwango cha sukari mwilini pamoja na homoni ya insulini. Vitu vyote hivi kwa pamoja endapo vitazidi mwilini huufanya mwili kua katika hatari ya kupata magonjwa na kuharibu afya ya uzazi kabisa.
6;Mazoezi humfanya mtu kua na umbo zuri na la kikakamavu hivyo kumvutia mwenza wake. Mwonekano mzuri wa mfanya mazoezi humpa hali ya uwaminifu katika kushiriki ntendo la ndoa.

“FANYA MAZOEZI JENGA AFYA YAKO.”

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center