Fahamu kuhusu homa ya uti wa mgongo kwa watoto

Homa ya uti wa mgongo ni nini?

Ugonjwa wa uti wa mgongo(meningitis) ni uvimbe(infamattion) unaotokea kwenye tando zinazofunika na kulinda ubongo na uti wa mgongo

Dalili zake ni zipi?

Maumivu ya kichwa na nyuma ya shingo

Shingo kukaza

Homa kali

Utosi kuvimba

Kushindwa kustahimili mwanga(photophobia)

Degedege

Kutapika

Kulia kupita kiasi kwa muda mrefu hata baada ya kubembelezwa

Kushindwa kula na kunyonya

Dalili hizi pia zinaweza kuambatana na vipele, muwasho, mwili kuwa mdhaifu sana kuelekea kupoteza fahamu, kizunguzungu.

Dalili zikiambatana na upele chukua tahadhari kwa kumuwahisha hospitali kwani inaweza pelekea mlipuko wa ugonjwa huo kwa walio jirani kwa sababu husambaa kwa njia ya hewa

Uonapo dalili hizi kwa mtoto wako, muwahishe kituo cha afya apate matibabu kwa wakati.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center