Je,ninasafisha kinywa changu vizuri?

“Kinywa cha binadamu kwa kawaida kina mamilioni ya bakteria ambao hawana madhara yoyote hadi pale ambapo patatokea mabadiliko na kusababisha ya madhara tofauti.

Bakteria hawa hupatikana kwenye meno,ulimi na sehemu zingine za kinywa.

Usafi hafifu wa kinywa hupelekea matatizo kama meno kutoboka na matatizo mengine ya fizi.

Unaposafisha kinywa vizuri unaondoa hali tofauti zinazoweza kusababisha bakteria hawa kushambulia kinywa chako.

Jambo la msingi la kuzingatia ni kwamba usafi wa kinywa haujalishi tu ni mara ngapi unapiga mswaki bali ni kwa jinsi gani unapiga mswaki vizuri inavyotakiwa(effectiveness)

Mambo ya kuzingatia wakati wa kupiga mswaki;

Tumia mswaki laini

Dawa ya meno yenye madini ya floridi

Namna sahihi ya kupiga mswaki(correct brushing action)

Kupiga mswaki kwa mda usiopungua dakika mbili

video fupi  inayoelezea jinsi ya kupiga mswaki vizuri

Play Video

Hatua za kusafisha meno ni kama zifuatavyo;

1.  Weka mswaki wako katika degree 45 na meno yako ili mswaki wako ugusane na meno yako pamoja na fizi.

2. Sugua sehemu ya nje ya meno yako 2-3 taratibu bila kutumia nguvu kwa mwendo wa kuzungusha kisha sogea kwenye meno mengine 2-3 na rudia ivo ivo

3 .Endelea vile vile kwa meno ya ndani, mswaki ukiwa kwenye degree 45 na meno yako kwa mwendo wa kuzungusha mbele na nyuma kwenye meno na fizi zote.

4 .Geuza mswaki wako nyuma ya meno ya mbele kisha kwa mwendo wa kwenda juu na chini safisha meno hayo vizuri.

5. Weka mswaki wako kwenye sehemu ya meno ya kutafunia na kwa taratibu safisha sehemu hizo kwa mwendo wa kwenda nyuma na mbele.

6.  Malizia kwa kusafisha ulimi vizuri.

“kinywa chako ndio ufunguo wa mwili wako.”

Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku baada ya mlo wa asubuhi na baada ya chakula cha usiku.
Badilisha mswaki wako kila baada ya miezi mitatu na pale ambapo itakua imechanua. Muone daktari wa meno mara kwa mara kwa uchunguzi na matibabu ya mapema.

1 thought on “Je,ninasafisha kinywa changu vizuri?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center