Maambukizi ya Sikio la Kati (otitis media)

je wajua?

Kimsingi Sikio la mwanadamu limegawanyika kwenye sehemu kuu 3, sikio la nje, sikio la kati na sikio la ndani.

Maambukizi ya sikio la kati hutokea pale virusi au bacteria wanaposababisha mabadiliko nyuma ya ngoma ya sikio (Inflammation) yanayojumuisha uvimbe, maumivu, wekundu, joto na kuhafifisha utendaji kazi wa sikio la kati.

Hali hii huwapata sana watoto hasa majira ya baridi na mara nyingi huisha yenyewe pasipo matibabu, Ingawa ni muhimu kutafuta matibabu pale maumivu yanapozidi au homa kutokea.

Maambukizi ya sikio la kati yaweza kuwa ya haraka (muda mfupi) lakini yenye kuathiri uwezo wakusikia kutokana na majimaji na usaha unaojikusanya kwenye sikio la kati, mara nyingine majimaji na usaha huendelea kuongezeka hata baada ya maambukizi kutoweka na hivyo kumfanya mtu kushindwa kusikia kabisa.

Nini Kinasababisha Maambukizi ya Sikio la Kati?

Mara nyingi husababishwa na kusambaa kwa maambukizi yaliyo kwenye njia ya hewa kwenda kwenye masikio. Pale mrija unaounganisha sikio la kati na sehemu ya koo la hewa (mrija wa eustachian) unapoziba, majimaji hujikusanya nyuma ya ngoma ya sikio na kutoa nafasi kwa Bacteria kukua na kuleta mabadiliko yaliyoelezwa hapo awali

Mrija huu huziba kwa urahisi kwa watoto wadogo kwa sababu ya kuwa mwembamba, laini na usio wima, tofauti na kwa watu wazima ambapo huwa mpana, imara na ulio wima

Maelezo kuhusu dalili, matibabu, na namna ya kujikinga na maambukizi ya sikio la kati yataongelewa katika machapisho yanayofuata

4 thoughts on “Maambukizi ya Sikio la Kati (otitis media)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center