Fahamu kuhusu Kwashiorkor

kwashiorkor ni nini hasa?

  • Huu ni ugonjwa unaosababishwa na upungufu wa protini mwilini.Kuna magonjwa mengi ya utapiamlo na kwashiokor ni moja wapo
  • Magonjwa haya hupata watoto kwa ujumla na haswa wale walio chini ya miaka mitano

Dalili zake ni zipi?
1)Kushindwa kukua kwa mtoto kulingana na umri wake(Failure to thrive)
2)Kukonda kupita kiasi
3)Tumbo kujaa kupita kiasi na miguu kuvimba
4)Nywele kunyonyoka na kubadilika rangi (kama dhahabu)
5)Mabadiliko ya ngozi,huwa kama inabanduka na kuwa na vidonda
6)Mtoto huchoka haraka na kukasirika kirahisi
7)Mtoto kuugua mara kwa mara kutokana na kushuka kwa kinga ya mwili

“Close to a billion people,one-eighth of the world’s population still live in hunger.Each year 2 million children die through malnutrition.”  -Jonathan Sacks

  1. Nini cha kufanya?
    Kuwahi kituo cha afya kupata vipimo(kama vya mkojo na damu) vitakavyohakiki kuwa ni kweli mtoto ana upungufu wa protini mwilini
  2. Matibabu
    Kikubwa ni kumpa mtoto vyakula vya kuongeza nguvu na protini kwenye mwili wa mtoto,pia kutumia virutubisho vyenye protini ili kupunguza dalili na ukali wa ugonjwa

        Vyakula vinavyoongeza protini ni kama;                     Nyama,samaki,maziwa,maharage,njegere,jibini,mayai,karanga n.k

       Daktari atakuelewesha namna ya kula na ratiba ya kula ili mtoto apate nafuu haraka iwezekanavyo hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuwahi kituo cha afya

       Kama tiba itapatikana mapema mtoto anaweza akaendelea na maisha yake na ukuaji ukarejea kama kawaida

       Lakini kuna uwezekano mkubwa wa mtoto kupata shida ya ukuaji wa mwili na akili kama tiba itacheleweshwa,madhara mengine ni makubwa hata kupelekea kupoteza maisha

2 thoughts on “Fahamu kuhusu Kwashiorkor

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center