Je ugonjwa sugu wa figo ni nini?

Ugonjwa sugu wa figo  ni  kupoteza  kwa utaratibu  kazi ya figo ambao huchukua miezi hadi miaka.

Kazi ya figo zako ni kuchuja uchafu na maji  zaidi kutoka kwenye damu, ambao huo uchafu unapeleka  unatoka moja kwa moja kwenye mkojo wako.

Ugonjwa sugu wa figo ikifika hatua ya juu, ngazi za hatari  za maji,electrolyes na uchafu  hujikusanya kwenye mwili wako.

Dalili za ugonjwa sugu wa figo

Dalili za ugonjwa sugu wa figo huanza kutokea pale figo zikianza  kuharibika taratibu

 • Kichefuchefu
 • Kutapika
 • Kupoteza hamu ya kula
 • Matatizo ya usingizi
 • Uchovu na udhaifu
 • Mabadiliko katika kiwango cha mkojo
 • Kupungua kwa umakini
 • Misuli kukaza
 • Kuvimba kwa miguu
 • Kuwashwa
 • Maumivu ya kifua
 • Kukosa pumzi
 • Shinikizo la damu

Hakuna dalili maalum za magonjwa za figo , maana yake  hizi dalili pia zinaweza sababisha na magonjwa mengine.

 

    Magonjwa unayosababisha ugonjwa sugu wa figo.

 • Kisukari
 • Shinikizo la damu
 • Magonjwa ya figo kama vile Glomerulonephritis, interstitial nephritis , polycystic kidney disease
 • Kuziba kwa muda mrefu njia za mkojo, kutokana na kuvimba kwa tezi dume, mawe ya figo  na baadhi ya kansa
 • Maradhi ya figo mara kwa mara

Visababishi hatari  ni kama:

 • Kisukari
 • Shinikizo la damu
 • Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu
 • Uvutaji wa sigara
 • Uzito uliopitiliza
 • Historia katika familia kuwa na ugonjwa wa figo
 • Figo isiyo ya kawaida kwa kimaumbile
 • Umri mkubwa

Madhara ya ugonjwa sugu wa figo

Ugonjwa sugu wa figo huweza kudhuru sehemu yeyote ya mwili wako.

Baadhi za madhara ni:

 •     Maji yanoshindwa kutoka mwilini hupelekea kuvimba kwa miguu na mikono
 •       Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu
 •         Mifupa kulegea hivyo kupelekea mifupa kuvunjika
 •     Upungufu wa damu mwilini
 •    Kupunguza  nguvu za kiume
 • Hupunguza kiinga ya mwili, hivyo pelekea mgonjwa kupata hatari ya mwili kushinda kujilinda na maambukizi mpya.
 • Ikifika hatua za mwisho wa figo kuharibika , mgonjwa anahitaji kufanyiwa usafishaji wa figo(dialysis) au kupewa figo jingine(kidney transplant).

Jinsi ya kujizuia kupata magonjwa ya figo

Ni kawa njia zifuatazo:

 • Fuata maelekezo ya dawa unazopewa.Baadhi ya dawa huweza haribu figo yako.
 • Kuwa na uzito wa afya. Kama una uzito uliopitiliza ,punguza uzito kwa kufanya mazoezi na kupunguza chakula.
 • Usivute sigara . Uvutaji wa sigara huweza kuharibu figo zako na kufanya hali iwe mbaya zaidi.
 • Kama una ugonjwa ambao huweza kuwa sabibishi ya figo kuharibika , jua jinsi yakumudu ugonjwa huyo na daktari wako.

Utambuzi wa ugonjwa wa figo ni kwa vipimo vifuatavyo

 • Vipimo vya damu
 • Vipimo vya mkojo
 • Ultrasound

Matibabu:

Matibabu ya ugonjwa sugu wa figo  hulenga katika kupunguza kuharibika kwa figo, kwa kudhibiti sababu ya msingi.

Ugonjwa sugu wa figo huweza enedelea kufikia hatua ya mwisho ya figo hushindwa kufanya kazi ,Mtu huitaji  usafishji wa figo(dialysis) au kupandikiziwa figo(kidney transplant)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center