Ukosefu wa choo(constipation) na tiba asilia

 

Hali ya kukosa choo ni tatizo linalokumba asilimia kubwa ya watu. Kisayansi,  Unapopata choo chini ya mara 3 kwa wiki, inatosha kusema una hali ya ukosefu wa choo (constipation). 

ukosefu wa choo husababishwa na vitu mbali mbali, hususani ;- 

i)kula vyakula vikavu mfano mkate, biskuti n.k

ii)kutopata vyakula vinavyo saidia mmeng’enyo mzuri wa chakula mfano matunda kama ndizi

iii)madawa mbali mbali

iv)magonjwa mfano uvimbe tumboni, vidonda vya tumbo.

Ukosefu wa choo huambatana na baadhi ya dalili kama tumbo kujaa gesi, tumbo kuuma, kupata choo kigumu na kikavu ambacho husababisha maumivu muda wa kujisaidia.

Kuna njia mbali mbali asilia za kupunguza hali ya ukosefu wa choo, ambazo waweza zitumia uwapo nyumbani. Nazo ni kama zifuatazo;-

1)Kunywa maji kwa wingi

2)Ulaji wa mboga mboga na matunda kwa wingi

3)Fanya mazoezi ya viungo kwa wingi

4) Kunywa kahawa kwa wingi

5) Tafuna majani ya senna

6) kunywa mafuta ya mnyonyo

7) Epuka unywaji wa maziwa kwa wale wasioweza meng’enya maziwa mwilini mwao.

Kama tatizo la ukosefu wa choo litaendelea kwa muda mrefu pamoja na kutumia njia tajwa hapo juu basi fika hospitali kwa uchunguzi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center