Nini husababisha madhara ya afya kutoka kwenye tumbaku

Sigara hutengenezwa na majani yaliyokaushwa ya zao la Tumbaku na kwenye zao hilo ndipo hupatikana kemikali zijulikanazo kama ‘tar’ na ‘nikotini’, kaboni monoxaidi, ammonia, DDT nk. Pia huweza kuongezewa ladha za aina mbali mbali ili kuvutia wateja.

Watu wengi kwa muda mrefu hudhani kua Nikotini ndio inayosababisha kansa. La hasha, Nikotini husababisha kushindwa kuacha sigara kwa kiurahisi (addiction). Nikotini huongeza hamu ya kutaka kuvuta sigara mara kwa mara. Tumbaku imetengenezwa na kemikali nyingi tofauti zaidi ya sabini ambazo huweza kusababisha kansa. Kemikali aina ya Tar ndio inayosababisha kansa kwa kiasi kikubwa. Huonekana kama gundi ya rangi ya udongo.

Tukiongelea madhara ya tumbaku mwilini, moja kwa moja tunazungumzia madhara ya uvutaji wa sigara. Madhara hayo ni:

  • Upofu katika uzee.
  • Uume kushindwa kusimama.
  • Mimba kutungwa nje ya mfuko kizazi (ectopic pregnancy).
  • Kutengua kiuno na mifupa.
  • Saratani ya utumbo mkubwa.
  • Homa ya mifupa (rheumatoid arithritis).
  • Watoto kuzaliwa na mdomo sungura (cleft palate).
  • Matatizo katika kizazi.
  • Magonjwa ya mdomo (fizi na meno).

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center