Nifanye nini ili nipate mapacha?

" Je, nifanyeje?

Ni ndoto ya wanawake wengi kupata watoto mapacha na hii imepelekea swali hili kuwa swali la kila siku la wanawake wengi kwa madaktari mbalimbali.

Ukweli usiofichika ni kwamba hakuna njia madhubuti iliyopo ambayo inaweza kumfanya mtu awe na uhakika wa kupata watoto mapacha. Swali ambalo wanawake wanatakiwa kuuliza ni “Je, ni vitu gani vinavyoweza kuongeza uwezekano wa kupata mapacha?”

Kuna njia na vitu mbalimbali ambavyo iwapo vitafanywa kwa kujua au kutokujua huweza kuongeza uwezekano wa kupata mapacha. Na baadhi ya njia hizi ndio huweza kujibu baadhi ya maswali ya kwanini mtu amepata mapacha na kwanini hajapata.

 

twin 4

Je, ni vitu vinaweza kuongeza uwezekano wa kupata mapacha?

1.Kuwa na historia ya uzao wa mapacha katika familia.

-Takwimu zinaonyesha kuwa familia zenye mapacha hasa wasiofanana (fraternal) wana uwezekano mkubwa wa kuwa na uzao wenye mapacha tena.

2.Kuzaa ukiwa na umri mkubwa.

-Wanasayansi wamegundua kuwa wakina mama wengi wanaoshika ujauzito wakiwa na umri wa miaka 35 au zaidi huwa na uwezekano zaidi wa kupata mapacha kuliko wenye umri chini ya hapo. Sababu inayopelekea hii kutokea ni mwanamke anapokaribia ukomo wa hedhi, mwili wake hutoa yai zaidi la moja kila mwezi sababu ya ongezeko la homoni kipindi hicho.

3.Matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango.

-Vidonge vya uzazi wa mpango huchanganya mfumo wa kawaida wa homoni hivyo pale tu mwanamke anapoacha kutumia vidonge hivi mwili wake unakuwa bado upo kwenye taratibu za kurudi katika hali ya kawaida na hivyo kuwa na uwezekano wa kutoa mayai mawili katika mzunguko mmoja.

4.Kutumia dawa za uzazi (fertility drugs) au kupandikiziwa kiinitete (embryo).

-Takwimu zinaonyesha kuwa dawa za uzazi huongeza uwezekano wa kupata mapacha kwa asilimia 25 kwa kuongeza idadi ya mayai yanayotengenezwa na pia wakati wa kupandikizwa madaktari hupandikiza kiinitete zaidi ya kimoja ili kuongeza uwezekano pale ikitokea moja likashindwa kufanya kazi na hivyo kuongeza uwezekano wa mapacha.

5.Kuwa pacha.

-Wakina mama waliozaliwa kama pacha wana uwezekano mkubwa wa kupata mapacha.

6.Sababu nyingine ni kama kuwa mnene sana mwenye BMI zaidi ya 30 au kuwa mrefu sana na pia kuwa na asili ya uafrika.

jE, KUNA MADHARA YOYOTE YA KUBEBA MAPACHA?

Dalili za mjamzito mwenye mapacha hazina tofauti sana na mjamzito mwenye mtoto mmoja tumboni, Ila tu kuna baadhi ya dalili na vitu ambazo zitajitokeza kwa hali ya juu kwa mtu aliye na mapacha.

-Presha  kupanda wakati wa ujauzito.

-Upungufu wa damu.

-Kisukari cha ujauzito.

-Kutapika sana.

-Kuzaa kabla ya wakati (kabla ya wiki 38).

-Kuzaa watoto wenye uzito mdogo.

 

twin pics2

Kwa ujumla, hakuna njia madhubuti ambayo inaweza kufanya mwanamke apate mapacha na hivyo japokuwa kuna vitu vinavyoongeza uwezekano lakini hakuna chenye uhakika kwamba kukifanya au kuwa nacho utaweza kupata mapacha kwa asilimia 100 na njia zilizotajwa hapo juu kuna baadhi zina madhara kwa mwili hivyo ni heri kusubiri bahati yako.

1 thought on “Nifanye nini ili nipate mapacha?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center