Vitu Vitano Muhimu Kuhusu Kujifungua kwa Upasuaji

Kujifungua kwa upasuaji kunaongezeka kwa kasi duniani. Ongezeko hili linahusishwa kwa kiasi kikubwa na sababu nyingine mbali na za kiafya. Mfano uwoga wa maumivu wakati wa kujifungua kwa njia ya kawaida nk

Fahamu

KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI KUNAWEZA KUWA SALAMA ZAIdi.

Sababu moja kuu ya kujifungua kwa upasuaji ni mtoto kutokaa vizuri.

Pia pale kondo la uzazi linapoziba njia ya kutokea mtoto,haiwezekani kujifungua kawaida na mama na mtoto wanaweza tokwa na damu sana.

hatari zinazoweza ambatana na upasuaji.

Kupoteza damu nyingi wakati wa upasuaji, Kupata maambukizi mbalimbali. Kujeruhiwa viungo vingine vya mwili.nk

Pia mtoto anaweza pata majeraha na kuhitaji masaada wakupumua.

maumivu ni maKali zaidi

Watu wendi hupendelea kujifungua kwa upasuaji ili kuepukana na maumivu.

Upasuaji huambatana na maumivu ya muda mrefu zaidi na huleta shida wakati wa kuinuka, kucheka hata kupiga chafya.

KOVU

Mama hubaki na kovu baada ya upasuaji,Ingawa kovu linaweza kuwa dogo kutokana na mbinu za upasuaji.

Pale mama anapokuwa na mapacha au kuchelewa kufanyiwa upasuaji ,kovu linaweza kuwa kubwa. Hii huweza muathiri mama kisaikolojia na mapendo yake kwa mototo yakapungua.

huweza hatarisha mimba zinazofuata

Hii ni kutokana na uponaji wa kovu ndani ya kizazi, kanakwamba kondo la uzazi hujishikia ndani zaidi kwenye ukuta wa kizazi na huweza pelekea kutokwa na damu nyingi na kusababisha kizazi kutolewa.

Fanya upasuaji panapokuwa na ulazima kwa afya yako na ya mtoto.

6 thoughts on “Vitu Vitano Muhimu Kuhusu Kujifungua kwa Upasuaji

    1. Kitaalamu inashauriwa kujifungua mara tatu ili kuepuka madhara yatokanayo na upasuaji kwani huweza pelekea kushindwa kujifungua kwa njia ya Uke kutokana na uwezekano wa kupasuka kwa mfuko wa uzazi sehemu yenye kovu au kushindwa kujishika kwa kondo la uzazi.
      Ni vyema kujifungua mara tatu kwa upasuaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center