Fahamu ugonjwa unaoitwa Gout?

Gout ni aina ya uvimbe kwenye kiungio ambayo humpata  mtu yeyote. Inaweza  tokea kwa ghalfa kama maumivu makali,kuvimba, uwekundu katika viungo sanasana kwenye kidole kikubwa cha mguu .

Dalili

Dalili za gout zinaweza kuja na kuondoka , na huweza tokea kwa ghalfu na sanasana nyakti wa usiku

 • Maumivu mkali ya kiungo.

Sanasana kidole gumba cha mguu  na viungo sehemu nyiengine ya mwili kama vile magoti, kiwiko , kifundo cha mkono, na kifundo cha mguu.

 • Kuvimba na kuwa pekundu sehemu iliyoarthiriwa .
 • Kushindwa kutumia viungo kama ilivyo awali.

Sababu

Gout hutokea pale mawe ua urate zinajikusanya katika  sehemu ya viungo na hupelekea kuvimba na maumivu makali.Haya mawe ya urate hutokea pale ambapo kuna kiwango kikubwa cha  asidi ya uric mwilini kwenye damu.

Mwili wako kwa kawaida hutengeneza asidi ya uric baada ya kuvunja purines    ( zipo mwilini kiasilia)Hizi purines pia zinapatikana kwenye baadhi ya vyakula kama vile nyama nyekundu.Pia baadhi ya vinywaji vina sababisha kiwango cha asidi ya uric kupanda kama vile pombe  sanasana bia na vinywaji vya ladha ya sukari matunda ( fructose)

Kwa kawaida hii asidi ya uric huyenyusha ndani ya damu yako na hupita kwenye figo zako hadi kutoka nje ya mwili kama mkojo .Ila saa ziingine mwili wako unashindwa kutoa asidi ya uric mwilini hivyo mwishowe kutengenezwa kwa mawe ya uric asidi .Haya mawe ambayo hutengenezwa  ni makali, kama shindano hubaki  ndani ya viungo au tishu  inayozunguka hivyo husababisha  maumivu na uvimbe .

Vihatarishi

Unaweza pata gout kama una viwango vikubwa vya asidi ya uric ndani ya mwili wako.

Sababu zinaongeza kiwango cha asidi ya uric ndani ya mwili wako ni

 • Chakula

Kwa kula nyama nyingi, na kunywa pombe kama bia na kinywaji chenye sukari ya matunda .

 • Uzito uliopitiliza

Kama una uzito uliopitiliza , mwili wako hutengeza acidia ya uric zaidi ambapo figo kupata shida kwenye kuzitoa mwilini

 • Kuna baadhi ya magonjwa huongeza hatarishi ya kupata gout kama vile shinikizo la damu,kisukari, magonjwa ya moyo nay a figo.
 • Matumizi ya baadhi ya dawa.
 • Historia katika familia kupata gout.
 • Umri na jinsi.Gout huwapata sanasana wanaume kuzidi wanawake ni kwasababu miili ya wanawake hutengeza kiwango kidogo cha asidi ya uric
 • Upasuaji wa awali au ajali.

Madhara ya Gout

 • Gout ya mara kwa mara.
 • Gout ya  juu zaidi.
 • Mawe ya figo.

Jinsi ya kujikiinga

 • Kwa kunywa maji mengi ( angalau glasi nane za maji kwa siku moja).
 • Zuia au chunga kiasi cha pombe unachokunywa.
 • Pata protein yako kutoka kwenye vyakula viingine kama vile maziwa.
 • Chunga kiasi cha nyama unachokula.
 • Tunza uzito unaoendeana na urefu wako.

Ili kujua una gout kuna baadhi ya vipimo hufanyika kama vile

 • Vipimo vya damu.
 • X –ray.
 • Ultrasound
 • CT scan.

Matibabu

 • Hususani ni dawa na mabadiliko katika jinsi ya maisha.
 • Kujichunga kiasi cha pombe cha kunywa na vinywaji vyenye sukari ya matunda.
 • Kujichungua kiasi ya vyakula vyenye kiwango cha juu cha purine kama vile nyama nyekundu.
 • Fanya mazoezi mara kwa mara .
 • Kupunguza uzito.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center