Mfungo wa Kitabibu

Mtu anapopata ugonjwa, mara nyingi huanza kuwa na dalili kama vile homa, kuumwa kichwa nk ambazo huashiria kuwa kuna kitu hakipo sawa.

Katika wakati huu, mara nyingi ni vizuri kufunga.

Mfungo huu unahusisha kutumia tu maji na juisi ya limao au zabibu zisizochacha. Huweza kuwa mara nyingi kwa siku kadri utakavyojisikia!

Kumbuka kuwa mfungo wa kunywa maji tu si bora sana kuliko huu wa kunywa na juisi ya limao / zabibu

Mara zingine ni vizuri mfungo huu uendelee kwa muda wa siku 2 au 3, muda ambao mwili unakazana kupambana na ugonjwa ulioingia mwilini katika hatua za awali

Mara zingine ni vizuri kutumia tu juisi kwa siku kadhaa. Lakini wakati mwingine ni vizuri kutumia juisi kwa siku 1 au 2, kisha mlo laini kwa siku 2 au 3

Lakini kwa ujumla, waweza kuanza kula mlo laini baada ya dalili hizi mfano homa kuisha

Kufunga hupatia mwili nafasi ya kupumzika kifiziolojia. Mwili unapata nafasi ya kutoa nje ya mabaki ya vijidudu vilivyoshambuliwa na kinga ya mwili. Viungo vyote vya mwili vinajirudisha katika hali yake ya awali kabla ya ugonjwa.

Asili ya mwili ni tabibu wa kipekee. Pale mtu anapofunga, mfumo wa mwili unaanza kutumia virutubisho vilivyopo katika tishu za mwili. Hizi hutumika kuhudumia mahitaji muhimu ya mwili wakati uponyaji unaendelea.

Lakini tahadhari kuwa kufunga huhitaji umakini na maandalizi mazuri. Si njia inayofaa watu wote kwa ujumla. Mmoja aweza kufunga bila tatizo lolote, wakati mwingine aweza kuhangaika sana. Yule anayejisikia kuumwa kiasi kidogo atanufaika zaidi na njia hii. Lakini yule aliyezidiwa aweza kupata shida zaidi.

2 thoughts on “Mfungo wa Kitabibu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center