Vyakula vifaavyo kwa ajili ya mama anaenyonyesha

mama anaenyonyesha hupaswa kula aina gani ya vyakula?

Siri kubwa juu ya kunyonyesha ni kua, haijalishi utakachokula, mwanao hupata virutubisho vyote vinavyohitajika kwa ajili ya kukua. Haimaanishi kuacha kula vyakula vyenye virutubisho na kula mafuta zaidi. Kiasi kihitajikacho cha mafuta ni 300-500cal kwa siku. Kiasi hiki huhitajika kuongeza maziwa, kurudisha nguvu zilizotumika.

Wanasayansi wamegundua kua watoto wanaonyonya vizuri miezi sita ya kwanza na zaidi huwa na tabia ya kula vizuri katika umri wao wa miaka 6 ukilinganisha na wale ambao hawakunyonya vizuri.

Vyakula ambavyo mama anaenyonyesha huweza kutumia ni kama vile:

  • Maji masafi ya kunywa. Sio chakula bali husaidia kwenye utengenezaji wa maziwa na humsaidia mama kutokupungukiwa na maji na nguvu mwilini. Vimiminika ambavyo havijaongezewa ladha kama supu, mtori na juisi fresh huweza kusaidia kuongeza maji.
  • Samaki. Hii ni njia nzuri ya kupata protini. Samaki huwa na vitamini B12 na madini ya Omega-3 ambayo huweza kusaidia katika swala la sonona baada ya kujifungua (postpartum depression). Husemekana pia kua na madini ya vitamin D.
  • Nafaka zisizokobolewa. Huweza kupatikana kwenye mikate (brown bread), mchele, pasta, oatmeal nk. Huwa na vitamini B, madini na nyuzinyuzi (faiba). Huweza kusaidia kukufanya kujihisi umeshiba kwa muda, kukusaidia kupunguza uzito baada ya kujifungua na kufanya sukari yako ya mwili kuwa sahihi.
  • Nyama. Huhitaji madini ya Zinki kwa mama ni jambo la muhimu, na nyama ni njia sahihi ya kupata madini haya. Nyama pia hua na vitamini B na madini ya chuma.
  • Mayai. Hiki ni chakula cha haraka. Kina utajiri wa madini ya folate, vitamini B12 na D. kula yai zima ili kupata virutubisho kutoka kwenye pande zote mbili. Wanasayansi wamegundua kua mayai hayaongezi kolestelo kwa kiasi kikubwa.
  • Mboga za majani. Hizi hutupa virutubisho vingi na huwa na kiwango kidogo sana cha mafuta. Huwa na vitamini A, C, E na K na madini ya Kalsham na pia huwa na sifa ya kuondoa sumu mwilini.
  • Jamii ya kunde na maharaghe. Jamii hizi husemekana kua na protini ya kutosha na nyuzinyuzi (faiba), madini nk.
  • Karanga na mbegu. Hii pia ni njia nzuri ya kupata protini, faiba, vitamini, madini, vipunguza sumu mwilini, na mafuta mazuri mwilini. Huzuia magonjwa ya moyo, husaidia kuzuia kuzeeka mapema na ni nzuri kwa ngozi na kukusaidia kujisikia umeshiba.

Kila mama anaenyonyesha hupaswa kuzingatia mlo mzuri wenye virutubisho kwa ajili ya afya nzuri ya mtoto wake. Kunyonyesha kwa mama hukadiria/ hutabiri afya ya mtoto wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.