Fahamu zaidi juu ya kukoma kwa hedhi (menopause).

kukoma kwa hedhi ni nini?

Kukoma kwa hedhi ni pale mwanamke anapoacha kuona siku zake na hivyo kufanya apoteze uwezo wa kushika ujauzito tena kwa njia asilia.

Hedhi kwa kawaida huanza kupungua miezi au miaka kadhaa kabla haijaacha kiujumla. Mara nyingine hedhi huacha kutoka ghafla.

Kukoma kwa hedhi ni sehemu ya kawaida ya maisha ya mwanamke amabyo hutokea kati ya miaka 45-55. Hii husababishwa na kupungua kwa homoni za oestrogeni katika mwili wa mwanamke.

“Mwanamke 1 kati ya 100 hupata kukoma kwa hedhi kabla ya miaka 40”

Dalili za kukoma hedhi ni zipi?

Dalili ya mabadiliko ni katika mzunguko wako.

-unaweza kupata aidha hedhi nyepesi sana au nzito sana na pia unaweza kupata hedhi kila baada ya wiki 2 au 3 au hata mara moja kwa miezi kadhaa na mwishoni kuacha kabisa.
 

“Wanawake 8 kati ya 10 hupata dalili za ziada kwa muda kabla hedhi haijaacha kabisa”. Dalili hizi ni kama:-

-Hali ya kusikia joto kupita kiasi hasa maeneo ya uso, shingo na kifua.

-Kutokwa na jasho usiku.

-Kuwa mkavu ukeni na kutofurahia kufanya tendo la ndoa.

-Kupata shida kulala.

-Kuwa na hofu na hisia kushuka.

-Hamu ya kufanya tendo la ndoa kupungua.

-Kupata tatizo na kumbukumbu ya vitu na kutokuweza kufanya vitu kwa umakini kama mwanzo.

-Kichwa kuuma.

-Mapigo ya moyo kwenda mbio.

-Maumivu kwenye  viungio.

-Kupata maambukizi ya UTI mara kwa mara.

-Kukoma kwa hedhi huweza kupelekea mifupa kuwa dhaifu.

Black couple having a fight, man tries to say sorry but the woman won't talk
PIC: 123RF

Dalili hizi zinaweza kuanza miezi au hata miaka kabla hedhi kuacha kutoka kabisa na hukaa hata miaka minne baada ya hedhi ya mwisho.

Takwimu zinaonyesha kuwa “mmoja katika ya wanawake 10 huwa na dalili hizi hata kwa miaka 12”

je, kuna haja ya kumuona daktari?

Ni vyema kumuona daktari kama una dalili za kukoma hedhi zinazoathiri mwenendo wako wa kila siku wa maisha au kama umeanza kupata dalili hizi kabla ya miaka 45.

Matibabu haya yanalenga kupunguza dalili za kukoma kwa hedhi:-

-Daktari anaweza kukupatia vidonge vya kusawazisha homoni zako.

-Kukushauri kumuona mwanasaikolojia kama unapata hofu na hisia kushuka.

-Kula vyakula vyenye lishe bora na kufanya mazoezi mara kwa mara.

-Kuvaa nguo nyepesi, kuweka chumba katika hali inayoruhusu mzunguko mzuri wa hewa ili kupunguza kusikia joto na kutokwa na jasho usiku.

 

 

"ni muhimu kufahamu kwamba hali hii humkuta kila mwanamkwe na hivyo huna sababu na kuwa na huzuni wala hofu, ni kitu cha kujivunia"

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center