Inakuwaje Mimba Nyengine Zinapitiliza Muda

Je unajua urefu wa kawaida wa kubeba mimba kwa binadamu?

Kwa hali ya kawaida ,mwanamke hubeba mimba kwa muda wa wiki 37 mpaka 41.

Nani yuko kwenye kundi hatarishi kupitiliza muda wa kawaida

 1. Mimba za kwanza
 2. Wamama waliowahi kupitiliza muda katika mimba za awali
 3. Wamama wenye uzito mkubwa
 4. Wamama wenye mimba ya mtoto wa kiume

Ishara kuwa mtoto anepitiliza muda

 1. Kuwa na kucha ndefu
 2. Kuwa na nywele nyingi
 3. Ngozi kuwa kavu na legevu
 4. Kuwa na uchafu wa kijani au njano kutokana na kujisaidia tumboni

Athari kwa mtoto

 1. Kupungua kwa ukuwaji
 2. Kupata oxygeni pungufu
 3. Mtoto huweza kupaliwa na uchafu utokanao na kujisaidia
 4. Kupungukiwa kwa sukari kwenye damu kutokana na kutumia hifadhi yake yote.

Unajiepushaje?

Kuweka recorded vizuri ya siku ya kwanza ya mzunguko wa mwezi kabla ya kupata ujauzito itasaidia kugundua kama mtoto amepitiliza muda na kumuwezesha daktari kuchukua hatua husika.

Pia utumiaji wa ultrasound unaweza saidia kujua umri sahihi wa mtoto akiwa tunboni.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center