Fahamu namna za kumnyonyesha mtoto vizuri

Kunyonyesha ni jambo muhimu kwa mtoto hasa katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mtoto. Faida za kunyonyesha kama kujenga kinga ya mwili ya mtoto zimeelezwa katika makala zilizopita.

Katika makala hii tutaangalia ni jinsi gani mama anaweza kuhakikisha mtoto ananyonya vizuri bila shida. Hii inahusisha pande zote mbili, kwa mama na mtoto, jinsi ya kumweka wakati wa kunyonya kuhakikisha anamudu kunyonya vizuri

KWA UPANDE WA MAMA

  1. Mama anatakiwa kumweka mtoto karibu na kifua chake
  2. Mama anatakiwa kutazama ziwa upande anaonyonyesha
  3. Mama anatakiwa kumbeba mtoto kwa namna ambayo kichwa cha mtoto kitawiana na kiwiliwili chake katika mstari myoofu
  4. Mikono ya mama inatakiwa kusapoti vizuri mwili wote wa mtoto

 

KWA UPANDE WA MTOTO

  1.  Mdomo wa mtoto unatakiwa kufunika vizuri chuchu na sehemu kubwa ya duara jeusi linalozunguka chuchu(areola)
  2. Mdomo wa mtoto unatakiwa kupanuka kwa upana unaoweza kunyonya chuchu vizuri
  3. Kidevu cha mtoto kinatakiwa kugusa sehemu ya chini ya ziwa la mama

Ni vyema kuhakikisha mtoto ananyonya vizuri ili aweze kufaidika na faida zipatikanazo na maziwa ya mama, pia aweze kukua vizuri. Endapo mtoto anapata shida wakati wa kunyonya kwa kulia sana au kushindwa kupumua au kupata homa, muwahishe kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.