Njia asilia za kuzuia kiungulia

Kiungulia hutokea pale asidi zihifadhiwazo tumboni kwa ajili ya mmeng’enyo wa chakula zinapo toka na kupanda kuja kwenye njia ya chakula (esofagasi). Uwepo wa asidi hizi katika njia ya chakula husababisha maumivu makali yanayotaka kufanana na maumivu ya kuungua sehemu ya kifua ama kooni.

Tafiti zinaonesha asilimia kubwa ya watu wenye kiungulia wana ugonjwa kitaalamu unaoitwa “gastroesophageal reflux disease”-(GERD), pia kiungulia huonekana kwa wingi kwa wagonjwa wenye vidonda vya tumbo.ย 

Njia asilia za kupunguza kiungulia

.1) Epuka kula sana. –

Unapokula chakula kingi asidi hutolewa kwa wingi tumboni ambayo husababisha tatizo kuwa kubwa zaidi

2) Punguza unywaji wa pombe uliopindukia.

Pombe huongeza uwepo wa asidi tumboni, hupunguza uwezo wa valvu ya chini ya esofagasi kufunga hivyo kusababisha asidi kutoka tumboni kuingia kwenye esofagasi kiurahisi. Pia pombe hupunguza uwezo wa esofagasi kujisafisha na kuondoa asidi kwenye njia yake. Hizi zote hupelekea kiungulia.

3) Punguza utumiaji wa kahawa.ย 

Tafiti zinaonesha kahawa hupunguza uwezo wa valvu ya chini ya esofagasi kujifunga hivyo huongeza uwezo wa asidi kuingia kwenye esofagasi kirahisi ikitokea tumboni, hali hii hupelekea kupata kiungulia. Hivyo basi inashauriwa kupunguza utumiaji wa kahawa.

4) Punguza ulaji wa vyakula viongezavyo asidi tumboni mfano: matunda yenye juisi ya citrus mfano machungwa, malimao, vyakula viongezavyo gesi tumboni mfano maharagwe.

5) Punguza vinywaji vyenye gesi mfano soda kwani vinywaji hivi huongeza kiungulia

6) Kunywa maji kwa wingi. Maji husaidia kusafisha esofagasi kutoa asidi hivyo kupunguza kiungulia

7) Epuka kwenda kulala ndani ya masaa matatu baada ya kula chakula cha jioni.ย 

8) Jitahidi kulaza kichwa chako kwenye pembe ilioinuka. Njia hii hupunguza asidi kurudi kwenye esofagasi hivyo kupunguza kiungulia.

Endapo umetumia njia hizi zote na dalili za kiungulia zitaendelea bila mafanikio, fika kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.

Privacy Preference Center