Kuokoa macho yanayoharibiwa na kisukari!

Mara nyingi dalili za maradhi hujificha mpaka ugonjwa unafikia hali mbaya ambayo haiwezi kutibika. Hiki ndicho kinachotokea kwa ugonjwa wa macho unaosababishwa na kisukari. 

"Sikukata tamaa kupigania macho yangu"

Nilipoteza uwezo wa kuona kwa sababu ya kisukari mwaka 2004, lilianza jicho la kushoto na kisha la kulia. Bahati njema niliweza kuona tena japo kidogo baada ya upasuaji, sasa siwezi tena kusoma lakini walau nnaweza kuendesha gari na kujitegemea.

vitu vya kuzingatia

Muone daktari wako wa kisukari na pia wa macho kila kwenye kliniki kila mara. Usikose kliniki. Daktari atakusaidia kudhibiti ugonjwa wako na kugundua hatari nyingine zinazoweza kukupata. Pia tumia dawa unazopatiwa kiaminifu pamoja na kufuata ushauri wa madaktari. 

Pima macho yako mara kwa mara.  Kupima macho husaidia kujua kama uwezo wa kuona unazidi kupungua au la! Hii pia itasaidia kugundua maradhi mengine ya macho ambayo yatajeruhi zaidi macho yako. Unapogundua tatizo la macho mapema kwa kupima macho unaweza kupata tiba na kuzuia macho kupofuka au kudhoofika zaidi.

 

Dhibiti shinikizo la damu (blood pressure).
Hii pia inachangia kuharibu mishipa ya damu katika macho na hivyo kupelekea upofu zaidi.

Dhibiti kisukari. Uwezo wa kuona hupungua zaidi pale kiwango cha sukari inapokuwa juu. Macho yako yamedhooofika au kupofuka kwasababu ya kisukari. Amua kupambana na kisukari na macho yako yatabaki salama

“Unaweza kumpeleka ng’ombe bwawani lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji” mwili na afya ni yako itunze na kuijali. Watalamu wa afya hawatapambana vita hiyo badala yako. Ni lazima ushirikiane nao.

Katika kupambana na kisukari tunaokoa macho na kuepusha macho kuharibika zaidi kwa kisukari. Chakula na mazoezi ndio namna bora ya  kudhibiti kisukari na pressure ambao ndio maadui wakubwa wa ugonjwa huu wa macho. 

Unahitaji kupambana na kusikari na papo hapo kupata lishe bora na pia kufurahia chakula/mlo wako.

LISHE

Anza kutafuta vitu uvipendavyo ambavyo ni rafiki kwa afya yako. Muone mtaalamu wa chakula akuandalie mkakati wa lishe kulingana na upendeleo wako, uwezo wako wa kifedha na mahitaji ya mwili wako.

 

Kama ujumla waweza kuzingatia yafuatayo: Jitahidi sana Kula vyakula vyenye mafuta kidogo na sukari kidogo. Kula mboga za majani na matunda kwa wingi kuliko kawaida. Epuka juisi za viwandani na badala yake kunywa juisi asilia. Vyakula jamii ya maharagwe na jamii ya mizizi pia vinafaa. Kula nafaka zisizokobolewa. Pia epuka kukaanga chakula chochote. Kabla ya kupika jiulize… “nnaweza kuchemsha au kuoka hiki chakula?”

Mifano ya vyakula unavyopaswa kupendelea ni apple (an apple a day keeps the doctor away) maparachichi, broccoli, karoti, maharagwe, mboga mboga za aina zote, samaki au kuku wa kuchemsha, saladi za kila aina, matunda na vinginevyo. soma makala yetu juu ya chakula kinachofaa kwa wagonjwa wa kisukari.

Mazoezi

Mazoezi pia ni upande mwingine wa sarafu. Andaa utaratibu mzuri na rahisi kuufuata wa mazoezi. Utaratibu utakaoendana na kazi na shughuli zako. Ukiweka kipaumbele afya yako utaweza kutenga muda wa kushosha kufanya mazoezi kila siku. Ikumbukwe kufanya mazoezi kidogokidogo kila siku kuna faida zaidi kudhibiti sukari kuliko kufanya mazoezi makali kwa misimu. Tenga dakika 20-30 au zaidi kila siku kwaajili ya afya yako.

Vitu vya kuepuka

  • Acha kuvuta sigara. Na epuka kukaa sehemu zenye moshi (mf. jiko la kuni, viwanda vitoavyo moshi) Hii huchangia kujeruhi macho yako na kudhoofisha zaidi uwezo wa kuona.
  • Epuka kutumia vipodozi machoni, au vipodozi vyenye chemikali nyingi. Pia uepuka kutumia maji yenye chemikali za kuulia vijidudu mf. Maji ya swimming pool. Hakikisha umevaa miwani ya kuogelea.
  • Epuka kutumia nguvu nyingi kuona (eyestrain). Mf kusoma katika mwanga mdogo, au maandishi madogo, kusoma kwa muda mrefu.
  • Epuka vyakula vyenye sukari nyingi, mafuta mengi au wanga. Hata kama unajidanganya “ngoja ninywe soda alafu ntachoma insulin/ kunywa dawa”

“Unapopata dalili za kupungua uwezo wa kuona tayari kisukari kimeleta uharibifu mkubwa machoni. Hivyo chukua tahadhari zote kudhibiti kisukari na kupambana na upofu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center