Je, wajua athari za kisukari kwenye jicho?

Jinsi kisukari kilivyonipa upofu

Niligundulika na kisukari miaka 5 iliyopita. Madaktari walinipa dawa pamoja na ushauri juu ya vyakula. Kutokana na kukosekana kwa fedha ya kununua dawa, sikuweza kuzingatia utumiaji wa dawa. Sasa nina miezi 2 ambapo macho yangu yote mawili hayaoni kabisa.

Kisukari huharibu vipi macho?

Watu wenye kisukari huweza kupata na ugonjwa wa macho uitwao sukari ya macho. Sukari inapokuwa kwa wingi, huaribu mishipa midogo midogo ndani ya jicho inayoshughulika na usambazaji wa damu jichoni. Hali hii huaribu uwezo wa kuona wa jicho taratibu na endapo usiposhughuliwa mapema huweza pelekea jicho kushindwa kuona kabisa.

Dalili za kisukari kinapoathiri macho

Kuona kama matone au mistari ya rangi nyeusi ikielea katika upeo wako wa uonaji

Kushindwa kuona vitu kwa usahihi hasa maandishi na maumboya vitu mbalimbali

Kushindwa kuona kwa kipindi kisha uwezo wa kuona kurudi kama mwanzo

Kushindwa kuona/kutofautisha rangi

Kuwa na sehemu katika uinaji ambapo huoni kitu/unaona nyeusi

Kushindwa kuona kabisa

"DHIBITI SUKARI YAKO, LINDA UWEZO WAKO WA KUONA"

3 thoughts on “Je, wajua athari za kisukari kwenye jicho?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center