Fahamu kuhusu udata (ankyloglossia/tongue tie)

Ili ulimi uweze kufanya kazi zake vizuri unabidi ufike katika sehemu zote za mdomo. Uwezo huu unafanya mtu aweze kuongea vizuri,kumeza chakula na hata kusafisha mabaki madogo madogo katika kinywa chake.

ulimi wa kawaida unavyoonekana

udata Ni nini?

Udata ni hali inayotokea pale ambapo ngozi(tissue) inayouganisha uvungu wa ulimi na sehemu ya chini ya mdomo(floor of the mouth) inayoitwa lingual frenulum kua na tatizo flani.

Inawezekana ikawa fupi au imeunganishwa karibu sana na sehemu ya mbele ya ulimi(tip of the tongue).

Aina mbalimbali za udata;

 

 • Aina ya kwanza huwa haionekani sana japokua ulimi hushindwa kuzunguka pande zote za mdomo
 • Aina ya pili hufananishwa na “eiffel tower”
 • Aina ya tatu huwa na umbo la moyo “heart-shape”

Udata ni tatizo ambalo hutokea kwa watu wengi  na kama lisipotibiwa mapema husababisha matatizo mbalimbali kwenye kinywa cha mtu. Kwa kawaida ulimi unatakiwa kukaa kwenye sehemu ya juu ya mdomo(palate) na hii ina mchango mkubwa katika ukuwaji wa taya ya juu ya kwenye kutengeneza umbo la uso.

Ikitokea sasa mtu ana udata,ulimi hushindwa kufika  katika sehemu ya juu ya mdomo na matokeo  yake  sehemu hii huwa ndogo na nyembamba  na kupelekea meno kuota  bila mpangilio mzuri.Kwasababu hii watoto wanaokuwa bila udata kutibiwa huwa na matatizo mbalimbali kama;

 1. ·         Kushindwa kutamka herufi kama “r” na”L”
 2. ·         Kuhema kwa mdomo(mouth breathing)
 3. ·         Maumivu kwenye taya
 4. ·         Kuoza kwa meno,fizi kuvimba na kuwa na nafasi kati ya meno ya mbele chini
 5. ·         Kukoroma wakati wa kulala.

Njia rahisi ya kugundua kuwa mtoto ana udata ni kutokana na mtoto kushindwa kunyonya vizuri (failure to latch well) na kung’ata ziwa badala ya kunyonya .vyote hivi husababisha mama kupata maumivi makali kwenye chuchu na hata kuvimba(mastitis).

picha kuonyesha tofauti kwenye kunyonya kati ya mtoto mwenye udata na asiye na udata

nini hasa matibabu ya udata

Matibabu ya udata yatafanyika pale tu kukiwa na shida yoyote lakini kama haileti madhara kwa mtoto kwenye kunyonya au kuongea huwa inaachwa hivyo hivyo.Matibabu yake yanahusisha kukata ile sehemu ya ngozi iliyokuwa fupi au nene sana ili kufanya ulimi uwe huru(lingual frenectomy).Yote haya hufanyika chini ya uangalizi wa daktari wa kinywa na meno.

2 thoughts on “Fahamu kuhusu udata (ankyloglossia/tongue tie)

 1. Mtoto wangu ana miezi 9 hv sasa na anaonekana kuwa na tatizo la UDATA (tongue tie), ni wakati gani sahihi wa kukata ili ulimi uwe huru?

  1. Karibu sana Daktari mkononi.
   Pole kwa tatizo lililompata mwanao.
   Muda sahihi wa kukata tongue tie ni pale ambapo mtoto anashindwa kunyonya vizuri pamoja na kushindwa kuongea vizuri.
   Ni vyema ukaenda hospitali ili aonane na mtaalamu wa kinywa na meno ili amchunguze vizuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center