Je, unajua hatari ya nyama ya nguruwe kiafya?

Nyama ya nguruwe ‘’kitimoto’’ ni miongoni mwa kitoweo kinachotumiwa na kupendwa na binadamu kwa wingi, bila ya kujua kuwa nyama hiyo inaweza kuwa na athari kubwa kwa afya ya binadamu. Athari moja wapo ni kama bindamu atakula nyama iliyo na mayai ya minyoo aina ya taenia solium 

Nguruwe hupata maambukizi ya minyoo hiyo kwa kula majani yenye mayai ya minyoo hiyo na mayai hukua ndani ya nguruwe na kuwa minyoo na hiyo minyoo hutaga mayai ambayo hukaa kwenye misuli(nyama) ya nguruwe.

Hivyo basi binadamu akila nyama yenye mayai hayo ambayo haikupikwa au kuandalaiwa vizuri basi na yeye anakuwa anapata maambukizi. Mayai hayo hukua kwenye utumbo wa binadamu na kuwa miyoo mikubwa na hutaga mayai na hayo mayai husambaa mwilini kupitia mishipa ya damu na kwenda kukaa sehemu mbalimbali za mwili kama kwenye ini na ubongo. Pia njia nyingine za kupata maambukizi ni kwa kutumia maji yenye mayai na pia kuwana hali duni ya usafi.

Mtu akipata maambukizi kwenye ubongo basi wengine hupata dalili na wengine huwa bila dalili zozote za maambukizi.

Dalili ambazo zinaweza kuambatana na maambukizi kwenye ubongo ni;

  • Kupata kifafa
  • Kichwa kuuma sana
  • Kupata kizunguzungu
  • Kuchanganyikiwa

Hivyo basi kinga ni muhimu kuliko tiba, kwani ukipata maambukizi ya minyoo hii kenye ubongo utahitaji kufanya vipimo vya gharama kubwa kama MRI ya ubongo na tiba yake ni ya muda mrefu.

Hivyo basi ili kujikinga kutokupata maambukizi hayo, mambo yafuatayo yazingatiwe;

  • Kuandaa nyama vizuri na kuipika kwa joto la kutosha mpaka kuiva ili kuua mayai.
  • Kuweka mazingira na vyanzo vya maji katika hali ya usafi
  • Kukagua nyama vizuri kabla ya kuitumia kuhakikisha haina mayai.
  • Kupata dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu.

Privacy Preference Center