je kuna madhara ya kupiga punyeto(masturbation)?? mwanamke je??

Punyeto ni nini?? 

Kufanya au kupiga punyeto(masturbation) ni kitendo cha kutomasa sehemu zako mwenyewe za siri ili kujisisimua kimapenzi. Mtu anaweza fanya hivyo kwa kutumia vidole vyake(mkono) mwenyewe, au kujigandamiza sehemu baada ya kuona video za ngono au pia mtu anaweza kufanya kwa kutumia midoli(sex toys).

tafiti je?

Tafiti mbalimbali zinasema inakadiriwa Zaidi ya 95% ya wanaume wote walishawahi kupiga punyeto na zaidi ya 89% ya wanawake pia walishawahi kufanya tendo hili

mawazo ya jamii

Kwa muda mrefu sana kumekua na mitazamo tofauti kutoka katika jamii mbali mbali kuhusiana na swala hili, wapo wanao amini kua ni mwanaume tu ndo anapiga punyeto(ana masturbate) lakini ukweli ni kwamba kila mtu mwanaume na mwanamke  anaweza kupiga punyeto.

Mtazamo wa jamii kuhusiana na punyeto(masturbation)

Jamii mbalimbali zmekua na mtazamo tofauti juu ya tendo hili.

  • Wapo watu wanao amini kua punyeto ni ngono salama kwao kwa sababu kwanza haina gharama, haipotezi muda, na pia haina hatari ya kukupa maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama ukimwi na mengine yajulikanayo.
  • Wapo watu wanaopinga vikali kabisa swala hili la punyeto kwa kuamini kua ni ishara ya uchafu, kujiaibisha ย na pia ina madhara mengi sana na hivyo kuiona punyeto kama haramu.
  • Jamii za kidini zinaipa uzito punyeto sawa na tendo la kujamiiana kabsa.

Mtazamo wa kisayansi juu ya punyeto.

IZamani kisayansi punyeto ilikua inaonekana kama ni moja ya vitu vinavyofanywa na wagonjwa wa akili(psychological problems) lakini kwa sasa sayansi inaitazama punyeto kama sehemu ya ngono salama isiyokua na madhara yoyote endapo itafanywa kiutaratibu na sehemu sahihi.

Lakini pia punyeto imekua kama sehemu ya tiba kwa watu wanaowahi kufika kileleni(pre mature ejaculation), pia kuna baadhi ya vipimo ambavyo vitahitaji mbegu za kiume hivyo njia rahisi ya kupata mbegu hizi ni kwa kufanya punyeto.

Je kuna madhara yoyote ya kiafya au kijamii yatokanayo na kufanya punyeto(masturbation)??

Kila kitu kikizidi kiasi ni hatari. Japokua tafiti mbalimbali za kisayansi zinasema kua punyeto ni ngono salama isiyokua na madhara.. lakini hii ni pale tu endapo mtu ataifanya kwa utaratibu na kiasi.

Endapo mtu atafanya punyeto kupita kiasi ย atakua katika hatari ya kupata madhara yafuatayo.

  1. Kwa sababu punyeto hufanywa kwa kujichua kwa mkono, mtu anaweza kwana kupata michubuko ya ngozi ya juu ya uume na pia kuchua kwa nguvu na kuupindisha uume kwa nguvu kunaweza kusababisha kuharibika kwa chemba za kuzaja damu katika uumeโ€ฆ hii huleta matatizo baaae.
  2. Endapo mtu ย utazoea sana kupiga punyeto inaweza kukufanya ukawa unakatisha hata shughuli za maana kisa tu unataka kufanya punyeto. Kwa mfano mtu anaweza hata akatoka darasani , akasitisha shughuli zake za kila siku, kasitisha hata muda wa kua pamoja na ndugu na jamaa kisa tu anataka abaki pekeake ili aweze kufanya punyeto.
  3. Baadhi ya watu wanaofanya punyeto kupita kiasi husahau kabisa habari ya kua na mweza wa jinsia tofauti kwa kuamini kuaย  na mwenza kimapenzi ni usumbufu mkubwa na wakati yeye anajitosheleza kitu ambacho ni kinyume na mtazamo wa jamii.
  4. Kuna baadhi ya watu baada ya kunogewa na tendo hili hujikuta wanafanya tuu kitu hiki bila hata kujali yupo sehemu gani, hivyo inapelekea kujivunjia heshima ndani na nje ya jamii yako.
  5. Baadhi ya watu waliofanya tendo hili kwa muda mrefu hupata shida sana au wakati mwingine kushindwa kabisa kuacha kitendo hiki pale wanapohijati kuacha mpaka wapate msaada wa daktari.
  6. Baadhi ya vitu vinavyotumiwa wakati wa kupiga punyeto kama mafuta, lotion, sabuni na sex toys husababisha michubuko na allergy kwa mwili wa mtumiaji.

Je unaswali lolote kuhusiana na mada yetu ya leo? ย Basi ย una swali tuulize kwa kucomment hapo chini au wasiliana na sisi moja kwa moja.

Privacy Preference Center