Je, nifanye nini baada ya kugundua kuwa nina ugonjwa wa zinaa?

Karibu tena mpenzi msomaji wetu katika makala zetu motomoto unazozipata kila siku ndani ya tovuti yako pendwa ya daktari mkononi. Siku ya leo tutajifunza hasa juu ya mambo muhimu ya kuzingatia pindi unapogungulika kuwa una ugonjwa wa zinaa. Twende pamoja, karibu!

Je, magonjwa ya zinaa ni nini?

Magonjwa ya zinaa (STDs) ni magonjwa ambayo huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa njia ya ngono isiyo salama. Magonjwa haya yamekuwa tatizo kubwa hasa miongoni mwa watu walio kati ya umri wa miaka 15-39. Kuna aina  nyingi za magonjwa haya lakini magonjwa kama kaswende(syphils), kisonono(gonorrhea), klamidia(chlamydia) na ugonjwa wa malengelenge katika sehemu za siri(genital herpes) ni baadhi ya magonjwa ya zinaa ambayo yapo sana katika jamii yetu.

Tatizo ni nini hasa?

Kwa kawaida pindi mtu unapogundulika kuwa na moja ya magonjwa haya ya zinaa huleta hali ya mfedheheko msongo wa mawazo na aibu, na pengine hali hii huchangiwa zaidi na namna ambavyo magonjwa haya huenezwa, ukizingatia hata jina lake ambalo linaonyesha kuwa yametokana na zinaa, hii ni tofauti na aina nyingine za magonjwa ya binadamu.

Nifanye nini sasa ninapogundulika nina magonjwa haya?

Kwa kawaida utambuzi huu hutokea katika mazingira ya hospitali baada ya mtu kwenda kutafuta huduma ya tiba, sasa basi unashauriwa kuzingatia mambo yafuatayo ili kujihakikishia kwamba unapona kwa uhakika na kuepuka maambukizi mengine.

  • Hakikisha unamaliza na kuzingatia matumizi dozi ya dawa utakazopewa hospitali, hata kama dalili za ugonjwa wako zitakuwa zimeondoka
  • Pia unashauriwa kumwambia mwenzi wako ili naye akapime na kama atakutwa na ugonjwa wa zinaa basi naye apate kutibiwa.
  • Epuka kujamiiana na mwenzi wako katika kipindi chote cha ugonjwa mpaka pale utakapokuwa umepona au nyote mtakapokuwa mmetibiwa na kupona kabisa hii itasidia kutopata maambukizi mapya ya ugonjwa wa zinaa.
  • Pia kama utaona dalili za ugonjwa mara baada ya kumaliza dozi ya dawa ulizopewa, basi wahi mapema ukamwone daktari ili ukapimwe kujua kama ugonjwa umerudi au kama ni maambukizi mapya hii itasaidia kupata tiba sahihi mapema.
  • Jambo la muhimu zaidi baada ya kupona hakikisha unakuwa mwaminifu kwa mwenzi mmoja pia epuka ngono zisizo salama(hakikisha unatumia kinga).

Timu ya daktari mkononi tunasema asante kwa kutoa muda wako kutembelea tovuti yetu, tungependa kukusihi usiache kutembelea kila siku pia mshirikishe na rafiki yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center