Je, Unafahamu kuhusu Saratani ya Uume

Saratani ya uume ni nini?

Hii ni aina ya saratani inayotokea haswa kwenye ngozi ya uume wa mwanaume . Wanaume ambao wana zaidi ya umri wa miaka 50 na kuendelea , Haswa wale ambao hawajatahiriwa.

Mabadiliko yana anzia wapi kwenye uume?

Mabadiliko  ya kwanza saratani hii inapotokea kwa mwanaume , Inaanzia  kwenye ngozi ya uume  zaidi kwenye  tezi (glans) au govi (foreskin) mpaka kwenye shimoni ya uume (shaft).

Dalili za saratani hii ni zifuatazo,

 • Kutokwa na uchafu wenye harufu chini ya govi(foreskin) kwenye sehemu za siri za mwanaume.
 • Mabadiliko ya ngozi ya uume , mara nyingi ngozi inakuwa nene kama imevimba.
 • Kidonda kisichopona (ulcer sore) takribani wiki nne mfululizo.
 • Kutokwa ma damu chini ya govi (foreskin).
 • Uume huota upele aina ya wekundu na uvimbe mwembamba wa rangi ya bluu kahawia.

 

Vihatarishi vya ugonjwa huu  ni vifuatavyo,

 • Uvutaji sigara uliokithiri na tumbaku ,tafiti zinaonyesha hivi ni vyanzo hatarishi vinavyoleta saratani hii kutokea.
 • Umri pia unachochea,  inakadiriwa wenye ugonjwa huu ni wale   waliokutwa na umri zaidi ya miaka 55 . Hata pia historia ya familia pia kupitia jeni (genes) inaweza ikapelekea mtu kupata saratani hii  , japo chanzo halisi cha saratani hii hakijulikani (idiopathic).
 • Kutotahiriwa, kunaweza kuwa chanzo cha ugonjwa huu  huleta maambukizi na mlundikano wa uchafu (smegma) unaochochea saratani hii kutokea.
 • Mambukizi ya ugonjwa kama HPV nayo ni kihatarishi tosha.

Je tunazuiaje saratani hii,

 1. kupunguza uvutaji wa sigara na tumbaku uliokithiri ,
 2. kutahiriwa mapema kabla ya umri mkubwa,
 3. kuzingatizia usafi maeneo ya sehemu za siri za uume ,
 4. kuepuka mambukizi ya ugonjwa wa HPV unaosababishwa na ngono nzembe.

Tiba ya saratani ya uume,

Inategemea na steji ya saratani , mara nyingi tiba huwa upasuaji ,matibabu kutumia miale , ma tibakemikali (chemotherapy)

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center