“Chikungunya” ugonjwa hatari leo Tanzania, Tuujue!

Homa ya chikungunya ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya chikungunya. Virusi hivi viligundulika mnamo mwaka 1952 Mtwara nchini Tanzania na viliweza kupatiwa jina kutoka lugha ya kimakonde ‘chikungunya’ maana yake ni ‘kilichopinda’ kutoka na mwonekano wa aliyekwisha kuambukizwa mwili wake hupinda kutokana na maumivu ya viungo vyake.

Je unaambukiza vipi?

Ugonjwa huu unaambukizwa na mbu, kama ilivyo kwa Malaria ila ni jamii tofauti. Jamii ya mbu wa Chikungunya ni ileile kama ya homa ya ‘dengue’ na ‘zika’ kitaalamu wanaitwa ‘Aedes aegypti’ na ‘Aedes albopictus’ ambao huuma mchana na usiku. Kwa mara chache sana huweza kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto au kuchangia na kugusana kwa damu.

Sasa zijue dalili

Baaada ya kuambukizwa kati ya siku 3-7 dalili huwa ni homa, maumivu ya viungo, maumivu ya kichwa, kuvimba viungio na vipele kama ilivyo homa ya dengue. Ugonjwa ukikomaa mwili huanza kupinda na kutembea kwa kuinama.

Matibabu inakuaje?

Kama ilivyo kwa virusi vingine huwa havitibiki, ila mgonjwa hupatiwa huduma na kurudi katika hali yake ya kawaida, na dalili zote kuisha. Inasemekana pia mtu huyu hupata kinga kutopata maambukizi tena.

Nitafanya haya ili kuepuka

Kuepuka kuumwa na mbu, na hata baada ya kuambukizwa ili visisambazwe na mbu kwa wengine. Kama ilivyo kwa Malaria; • Kutumia chandarua chenye dawa • Kupuliza dawa za mbu • Kupaka dawa • Kuvaa nguo ndefu kufunika miguu na mikono, hata kichwa. • Kupima na kutibiwa pindi mama akiwa mjamzito
Ni jukumu letu kwa pamoja kwa kushirikiana na wataalamu wa afya kulitokomeza hili gonjwa hatari, ili kudhihirisha kuwa lilitokea Tanzania, na Duniani kote kimakosa sio mahali pake. Fika vituo vya afya kupata kulijua zaidi gonjwa hili. Fatilia toleo lijalo kuhusu ugonjwa huu kwa ufahamu zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center