Jinsi magonjwa ya kinywa na meno yanavyoweza kuathiri afya ya mtoto wako

Kinywa ni sehemu muhimu sana katika mwili wa mtoto kwasababu ya kazi mbalimbali ambazo zinafanywa na kiungo hichi ikiwemo kula,kuzungumza,kuonyesha hisia kama kucheka au kulia na pia ni sehemu ambayo mtoto hutumia kwa kujiliwaza kwa mfano kunyonya vidole kungโ€™ata kucha na kadhalika.

Pia watoto hupenda kuweka kila kitu wanachokutana nacho mdomoni ,ni muhimu kujua jinsi ya kutunza vinywa vyao ili kuepuka magonjwa mbalimbali yanayoweza kuadhiri afya zao

Magonjwa ya kinywa na meno yanayowapata watoto wengi mara nyingi ni magonjwa ya fizi(periodontal diseases) pamoja na kutoboka kwa meno(dental caries).Magonjwa haya yanweza kuadhiri afya ya mtoto kwa namna nyingi sana;
  • Kutoboka kwa meno kunaweza kusababisha maumivu ambayo humafanya mtoto kushindwa kula vizuri.Hii hali humfanya mtoto kushindwa kupata viritubisho sahihi kwenye mlo wake.
  • Kutoboka kwa meno kunaweza kusababisha mtoto wako kupata maambukizi sehemu zingine za usoni na shingoni(dental abscess)ambayo husababisha uvimbe kutunga usaha,maumivu makali na homa.
  • Ajali kama kuanguka kunapelekea meno kung’oka kabla ya mda wake na hivyo inaweza kumpelekea mtoto kuchelewa kuota meno ya utu uzima na hivyo akapata shida hasa wenzie wakimcheka kuwa ana mapengo,hii pia inaweza kupelekea mpangilio mbaya wa meno ya ukubwani(malocclusion)
  • Magonjwa ya fizi huweza kusababisha mtoto kuwa na harufu mbaya mdomoni na hii humfanya akose amani na hata kujitenga na wenzake .Mtoto anapokosa kucheza na kukaa na wenzake (interaction) huathiri ukuwaji wake na huweza ata kumfanya mtoto achelewe kuongea.
  • Muonekano wa mtoto pia huharibika pale ambapo meno yake yanapotoboka sana(rampant caries).Hii inaweza kumfanya mtoto kukosa kujiamini na pia kushindwa kuongea au kucheka vizuri na hata wengine hukataa kwenda shule na hivyo kuhatarisha ukuwaji wao.

meno yaliyooza sana(rampant caries)

harufu mbaya ya mdomo inaweza kumfanya mtoto ajitenge na wenzake

uvimbe au usaha kwenye fizi(dental abscess)

Kinywa cha mtoto kinabidi kilindwe na kutunzwa vizuri kwa sababu ina mchango mkubwa kwenye afya ya mtoto kwa ujumla.Usafi wa kinywa huanza hata kabla ya meno kuota mdomoni ambapo mama hutumia kitambaa kisafi kusafisha fizi na ulimi wa mtoto.

Mtoto anapokuwa chini ya miaka sita mzazi au mlezi anatakiwa kumsafisha mwenyewe na kwanzia miaka sita hadi 9 mzazi au mlezi anatakiwa kumsimamia mtoto wake wakati anasafisha meno yake na kwanzia miaka 9 na kuendelea mtoto anaweza kusafisha kinywa mwenyewe.

Ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa afya ya kinywa ya watoto wetu inalindwa na kutunzwa vizuri ili waweze kuwa na tabasamu zuri pamoja na afya nzuri ya mwili pamoja na akili kwa ujumla.

1 thought on “Jinsi magonjwa ya kinywa na meno yanavyoweza kuathiri afya ya mtoto wako

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center