Fahamu kuhusu Kifafa kwa Watoto

Utangulizi

 • Kifafa ni ugonjwa unaowapata watoto hata watu wazima huku wagonjwa wapya wakiwa sanasana watoto chini ya miaka miwiwli na wazee juu ya miaka sitini na tano (incidence) japokuwa stadi zikionesha watu wazima wakipata ugonjwa huu kulinganisha na watoto kwa siku za karibuni.
 • Kwa kawaida seli za ubongo huwasiliana kwa mpangilio maalum, kuharibika kwa mfumo huu wa mawasiliano hufanya akili izidiwe nguvu na kuleta madhara yasiyohitajika kwenye mwili yatakayoelezewa hapo mbeleni
 • Huweza kutokea kwenye upande mmoja wa ubongo (partial seizures) au kuathiri pande zote mbili za ubongo (generalized seizures)
 • Watoto wengi walio na kifafa, dalili zao hukoma wakifika ukubwani

“For reasons that are not understood, depression both increases the risk for developing epilepsy and is also common among people with epilepsy who experience many seizures”   Dale Hesdorffer

Visababishi vya kifafa kwa watoto

 1. Maradhi mfano watoto wenye ugonjwa wa Down’s au usonji (autism)
 2. Shida katika ubebaji mimba wamama,muda wa kujifungua au wakati wa ukuaji kabla ya miaka mitano. Kama shida hii itaweza kuathiri ubongo basi kuna uwezukano wa mtoto pia kupata kifafa
 3. Ajali ya kichwa, kuvuja damu ndani ya kichwa n.k
 4. Kurithi kutoka kwenye familia
 5. Pia hata uvimbe ndani ya kichwa huweza sababisha hali hii

Dalili zake ni zipi?

Hizi huwa hutokea ndani ya sekunde chache mpaka dakika kadhaa, dalili hizi pia hutofautiana kulingana na aina ya kifafa

 1. Kukakamaa kwa misuli mwilini
 2. Kupoteza fahamu
 3. Kushindwa kupumua au kuacha kabisa kupumua
 4. Kutetemeka na hata kuanguka bila sababu yoyote
 5. Kushangaa na kuzubaa bila kujibu chochote
 6. Kutembea bila mwelekeo

Matibabu yake je?

Kuna umuhimu mkubwa wa kuwahi hospitalini kupata matibabu. Kwa mtu anayeonesha dalili za kifafa ni bora ukatumia mbinu zozote kumshauri atulie na huku ukiita msaada au kutafuta njia za kwenda hospitalini

 1. Kwanza ni matibabu kwa njia ya dawa (Anti-Epileptic Drugs).Hii utapewa kulingana na aina ya kifafa na dalili zinazooneshwa na mtoto wako(husaidia asilimia 70 mpaka 80 ya watoto wenye ugonjwa huu)
 2. Kuepukana na vitu vinavyoleta hali kama hiyo kama kutolala vizuri,stress kupita kiasi,
 3. Milo maalum (ketogenic diet) ambayo una wanga kidogo bali protini na mafuta ya kutosha imeonekana kuwa na matokeo mazuri kupunguza mara ngapi dalili zinatokea kwa mtoto
 4. Kupata matibabu ya tabia kwa sababu wengi wao huwa na shida kama hasira,
 5. Upasuaji unaweza fanyika kutoa sehemu yenye shida kwa aina inayoathiri sehemu tuu ya ubongo

Madhara yake

 1. Japo sio wote, elimu ya mtoto inaweza kuathirika na kifafa hata kupunguza uwezo wake wa kujifunza vyema kama wenzake
 2. Watoto wengine hushindwa kujichanganya na wenzao kwa kuogopa kupata dalili kama kuanguka au kukakamaa mwili wakiwa wanacheza na wenzao hivyo
 3. Kuna wengine huonekana wakiwa na uwezo uliopungua kujifunza lugha au kuwa na akiba ya kutosha ya maneno

Cha kufanya

 1. Kwanza ni kumwahisha mtoto kwenye kituo cha afya au hospitali atakapopatiwa huduma stahiki iwe ni dawa, ushauri wa kisaikolojia na kadhalika
 2. Kumpa moyo mtoto ajue wazazi/walezi mpo pamoja nae na kumsaidia kama ana shida yeyote anayoipata kutokana na ugonjwa huu mfano.anaogopa kucheza na wenzake kwa kuwa anachekwa kila anapoanguka n.k
 3. Kuhakikisha mtoto anakunywa dawa zake vizuri na kumweleza daktari kama kuna mabadiliko yeyote kwenye maendeleo ya mtoto

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center