Macho kutokutoa machozi na upofu

Xerophthalmia, ‘Dry eye’ hii ni hali inayotokea pale jicho linapoteza uwezo wa kuzalisha machozi ya kutosha au kutokuzalisha kabisa. Hali hii hutokea kwa sababu mfumo wa kuzalisha machozi unakuwa umeathiriwa.

Ukosefu wa vitamin A ni sababu kubwa katika hili.

Yes you can edit every single element.

ü  Ukosefu huu hutokea pale mtu asipokula vyakula vyenye vitamin A kama vile matunda na mbogamboga za kijani.

ü  Pia hutokana na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kushindwa kufanya ufyozaji mzuri wa vitamin A kutokana na sababu mbalimbali kama magonjwa.

Je mtu anayekosa uwezo wa kuzalisha machozi kutokana na ‘Xerophthalmia’ anapata matatizo gani?

Yes you can edit every single element.

ü  Kushindwa kuona vizuri wakati wa usiku

ü  Macho kuwa makavu

ü  Kupata vidonda kwenye jicho kwa sababu ya kukosa kilainishi ambacho ni machozi

ü  Pia anaweza kupoteza kabisa uwezo wa kuona

Yes you can edit every single element.

ü  Kupatiwa machozi ya bandia kuepusha jicho kuharibika

ü  Kupatiwa vitamin A

ü  Kutibu magonjwa mengine yanayoweza kusababisha hali  kuwa mbaya zaidi kama vile maambukizi ya vijidudu katika jicho

Je ni kwa namna gani unaweza kujikinga na ‘Xerophthalmia’?

ü  Kuhakikisha watoto wanapata dozi stahiki za vitamin A waendapo kliniki

ü  Kula vyakula vyenye vitamin A kwa wingi kama vile mboga za majani na matunda

Macho kukauka kutokana na ukosefu wa vitamin A inaweza kusababisha upofu kutokana na macho kukwaruzika kwa sababu ya machozi kukosekana hivyo vidonda vinavyopona husababisha makovu ambayo hupelekea kutokuona.

daktarimkononi

Serikali imejitahidi sana kuzuia upofu kutokana na tatizo hili lakini pia kila mmoja ni wajibu wake kujipatia elimu ya kutosha kuhusu ukosefu wa vuitamin A na madhara yake pia namna ya kujikinga.

DM

Usikose kufuatilia daktari mkononi ili kuzidi kujipatia maarifa mbalimbali kuhusu afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center