Sonona (depression) ni nini?

Sonona

Sonona ni ugonjwa ambapo mtu anakuwa katika hali ya kutokuwa na furaha na  huathiri jinsi mtu anavyojisikia , anavyofikiria na anavyofanya vitu vyake .

Sonona huweza huathiri mtu yeyote wa umri wowote haibagui mtu .

Mtu mwenye sonona anaweza pata shida katika kufanya shughuli zake za kila siku na saa ziingine kujiona sio wa thamani.

Sonona sio udhaifu .

-Hisia za huzuni

-Hisia za kububujika machozi

-Hisia za upweke

-Kutokuwa na matumaini

-Kuudhika upesi kitu kidogo.

-Kukata tamaa

-Kupoteza moyo wa kupenda kitu fulani kama ilivyo awali kama michezo

-Kupotezea hisia katika tendo la ndoa.

-Kukosa usingizi au kulala sana.

-Uchovu

-Kukosa nguvu kufanya shughuli ndogo

-Kuongezeka hamu ya kula na hivyo hupelekea kuongezeka uzito.

-Kukosa hamu ya kula na hupelekea mtu kupungua uzito

-Wasiwasi

-Kutokutulia sehemu moja .

-Kufikiria,kuongea kwa utaratibu

-Hisia za kutokuwa wa thamani.

-Kujilaumu

-Shida katika kufikiria , umakini na kufanya mamuzi.

-Fikra za kifo

-Fikra za kujiua

Baadhi ya watu  kujisikia vibaya au kutokuwa na furaha bila kujua sababu.

Watu wenye sonona dalili zake zina weza fika hali mbaya husababisha matatizo katika shughuli za kawaida za kila siku kama vile

-Kazi

-Masomo

– Mahusiano na wengine

 

-Uzito uliopitiliza huweza pelekea mtu kupata magonjwa ya moyo kama vile shinikizo la damu.

-Maumivu.

Utumiaji mbaya wa pombe

-Ugomvi katika familia, shida katika mahusiano na shule au kazini.

-Kujitenga na jamii

-Fikiria za kujiua

-Kujiumiza kama vile kujikata

 

Mfadhaiko utokano na maisha kama vile kupoteza ndugu wa karibu,shida ya kupata hela, kuonewa kwa kulazimiwa  au kuumizwa

-Historia ya ugonjwa wa akili kama  , matitizo ya kula , post traumatic disorder .

-Utumiaji wa kupindukia wa pombe au madawa ya kulevya

-Mabadiliko ya homoni.

Haswa katika kipindi cha ujauzito au baada ya kujifungua , baada ya kukoma hedhi.

-Historia ya ugonjwa wa sonona katika familia .

-Chukua hatua za kukabiliana na mfadhaiko wa maisha .

-Wafikie familia na marafiki wakati wa shida ili waweze kukusaidia .

-Mwone mshauri wa afya kwa ajili ya tiba .

1 thought on “Sonona (depression) ni nini?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center