Uume kusimama kupita kiasi (Priapism)

Uume kusimama ni jambo la kheri sana na pengine wanaume wengi hujivunia uwezo wao wa kusimamisha uume kwa muda mrefu. Habari hii inaweza kugeuka msiba kwa mhusika pale ambapo uume utaendelea kusimama bila yeye kutaka na kudumu hivyo kwa masaa kadhaa huku akipata maumivu makali. Ugonjwa huu hufahamika kama “priapism” na ni kati ya magonjwa yanayohitaji msaada wa haraka wa matibabu

Kwa kawaida uume husimama kwasasabu ya kujaa damu, damu ile hutakiwa kuingia na kutoka kupitia mishipa mbalimbali, mishipa hiyo inaposhindwa kufanya kazi yake vizuri hupelekea damu ile kujaa kupita kiasi na kukwama humo.

 

"Ugonjwa huu huweza kumpata mwanaume mwenye umri wowote hata watoto"

Dalili kuu tatu.

 • Uume kusimama kwa muda mrefu bila kukusudia na bila kupoa. (masaa manne au zaidi)
 • Maumivu kwenye uume,. Maumivu hayo huzidi kuwa makali muda unavyozidi kwenda.
 • Sehemu ya mbele ya uume(kichwa) hubaki laini    

Visababishi vya "Priapism"

 • Seli-mundu(sickle-cell). Ugonjwa huu ndio kisasabishi kikuu cha priapism. Kwasababu ya seli zenye sikoseli kuziba mishipa ya damu.
 • Baadhi ya madawa huathiri mishipa ya fahamu na mishipa ya damu ya uume na huzuia mishipa hiyo kufanya kazi vizuri. Mf. Dawa za kuongeza nguvu za kiume.
 • Madawa ya kulevya kama cocaine, bangi na mengine.
 • Majeraha kwenye uume yanaweza kujeruhi mshipa unaotoa damu kwenye uume na kusababisha kushindwa kupitisha damu vizuri.
 • Maradhi mbalimbali ya mfumo wa damu na baadhi ya cancer  pia huweza kusababisha ugonjwa huu.

Athari....

Pamoja na maumivu, uume unaposhindwa kupata mzunguko mzuri wa damu kwa zaidi ya masaa manne(4) seli zake hukosa mahitaji muhimu na kuanzia masaa sita(6) huanza kufa, hali hii ikiruhusiwa kuendelea kwa muda mrefu hupelekea seli nyingi zaidi kufa na hatimaye kupoteza uwezo wa uume kusimama kwa maisha yote.

Tiba!

Ni muhimu kupata kupata tiba mapema iwezekanavyo kwasababu madhara ya kudumu ya ugonjwa huu hayatibiki.
Matibabu  hufanyika hospitali kwa madawa, sindano za kupunguza damu kwenye uume na hata operesheni hasa baada ya masaa 6 tangu dalili zinapoanza.

Huduma ya kwanza (nyumbani)

 • Weka barafu kuzunguka uume na chini ya korodani. Hii itasaidia kupunguza maumivu na kuzuia damu kuendelea kukusanyika na kuleta shida zaidi.
 • Fanya mazoezi ya kupanda ngazi. Hii inaweza kusaidia kupunguza mkusanyiko wa damu katika uume    

Kumbuka!!!!

 • Ni muhimu kwenda hospitali haraka kwani muda unavyozidi kwenda ndivyo madhara ya kudumu yanendelea kukupata.
 • Ugonjwa huu husababishwa na vyanzo mbalimbali, hivyo ni muhimu kumueleza daktari historia nzima ya ugonjwa wako; jinsi ilivyoanza, kama hali hiyo imewahi kukutokea, kama umetumia madawa yoyote ya kuongeza nguvu za kiume, kama una ugonjwa wa seli-mundu(sickle-cell) na magonwja mengineyo ya kudumu.
 • Fuata masharti utakayopewa ili kuepusha kujirudia kwa ugonjwa na kupata tiba ya kudumu.

17 thoughts on “Uume kusimama kupita kiasi (Priapism)

 1. Thank you guys for the Knowledge your giving to us.. These helps even to have an idea on how to give a first aid to any victim at the spot

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center