Tatizo la kutokuona mbali

Ni nini hasa?

Hili tatizo ni pale ambapo machoย  hushindwa kuona vitu vilivyoko mbali lakini mtu huyo huweza kuona vitu vya karibu kwa vyema kabisa. Tatizo hili ni mojawapo kati ya matatizo ambayo yana asilimia kubwa sana ya waathirika ukilinganisha na matatizo mengi ya macho. Na watu wengi wanaovaa miwani hutokana na tatizo hili

Dalili zake ni zipi?

  • Kutoweza kuona vitu vya mbali kama alama za barabarani vyema
  • Kuona bila matatizo yoyote vitu vya karibu kama kusoma kitabu na kutumia simu ya mkononi
  • Kutumia nguvu kubwa sana ya kuona kwenye misuli ya jicho
  • Kupenda kufumba macho kidogo (kama unakonyeza) ili uweze kuona mbali kwa urahisi zaidi
  • Kuwa na tabia ya kuumwa kichwa mara kwa mara

Tiba yake ni nini?

  • Tiba kuu na rahisi ni kutumia miwani ya kusaidia kuona mbali ambayo hutolewa baada ya kwenda kwa daktari wa macho na kufanyiwa uchunguzi wa macho yako
  • Pia kuongeza kula vyakula/ matunda yanayoimarisha uwezo wa kuona kama karoti

Tatizo la macho kwa wazee

Tatizo hili huwapata watu ambao wenye umri mkubwa hasa wazee. Hupelekea kushindwa kuona hasa maandishi yaliyo karibu kama kwenye gazeti vizuri. Mtu hupenda kushika vitu mbali kidogo na macho ili aweze kuona maandishi vizuri. Tatizo hili ni la kawaida na hutokana na umri kusogea. Mzee mwenye tatizo hili, hupewa miwani ya kuona karibu ambapo humsaidia kuona maandishi vizuri bila shida yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center