Je!,wajua madhara ya shinikizo kubwa la damu kwa mama mjamzito?

          Habari ya kwako mpenzi msomaji wa Makala makini kabisa za afya, karibu tujifunze kuhusu afya ya mama mjamzito. Leo tutaangazia tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu kwa mama wakati wa ujauzito ( Gestational hypertension and pre eclampsia), madhara yanayoweza kusababishwa na tatizo hili na mambo ya kufanya ili kuepukana na  tatizo hili                                        Kupanda kwa shinikizo la damu kwa mama mjamzito( Zaidi ya 140/90 mmHg) huonekana kama jambo la kawaida, lakini ni tatizo ambalo huchangia vifo vingi kwa wajawazito hapa Tanzania. Kuna sababu nyingi zinazopelekea kupanda kwa shinikizo la damu wakati wa ujauzito; unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara, unene kupita kiasi,kutokufanya mazoezi kwa mama mjamzito, ujauzito wa mara ya kwanza, umri wa mama mjamzito [Zaidi ya miaka arobaini (40)] na mimba yenye motto Zaidi ya mmoja[ mapacha] huleta mgandamizo wa ziada na kusababisha shinikizo la damu kupanda                                                               Katika hali hii ya shinikizo kubwa la damu, mama mjamzito huwa katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo au vihatarishi vingine vya magonjwa ya moyo kama vile kisukari na kuganda kwa mafuta ndani ya mishipa ya damu  ( Atherosclerosis). Afya ya motto aliyeko tumboni huathiriwa kwa kiasi kikubwa na hata kupelekea kifo cha mama na mtoto aliyeko tumboni.                                                Ili kuhakikisha kuwa afya ya mama mjamzito inakuwa imara  wakati wa ujauzito na hata baada ya kujifungua, DAKTARI MKONONI inatoa ushauri kuwa ; Inampasa mama mjamzito kupima shinikizo lake  damu mara kwa mara kwa kutembelea kliniki ili achukue hatua stahiki za kuimarisha afya yake hasa anapojua kuwa ana shinikizo kubwa la damu. Pia ni vyema mama mjamzito afanye mambo yafuatayo ili aweze kuwa na shinikizo la kawaida la damu;

        KUFANYA MAZOEZI; kwa kweli mazoezi ni muhimu sana kwa afya ya mama mjamzito, ujauzito si ugonjwa bali ni hali tu ya muda yenye mibalaka mikubwa ndani yake, mama mjamzito asikae tu na kusubiri muda wa kujifungua ufike, Timu ya wataalamu wetu wa afya inashauri mjamzito afanye mazoezi madogo madogo kama vile kutembea kwa nusu saa na kufanya shughuli ndogo ndogo za nyumbani. Mazoezi haya yataimarisha afya yake na kumpatia nguvu zaidi.Pia mama mjamzito anashauriwa kutokuwa  na msongo  wa mawazo, suala ambalo huchangia kupanda kwa shinikizo la damu na kuathiri  afya yake pamoja na mtoto, anapaswa awe na furaha na Amani na awe katika mazingira rafiki yenye upendo na utulivu

KULA CHAKULA KIZURI; mama mjamzito asile vyakula vyenye mafuta mengi( hasa mafuta yatokanayo na wanyama) mara kwa mara , ni vyema kama akiachana navyo kabisa. Hii itamsaidia kuwa na shinikizo la kawaida la damu. Vyakula vya wanga, protini na vitamin kama vile matunda na mboga za majani ni muhimu sana kwa  afya ya mama mjamzito.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center