Kumbe mazoezi pia yanaweza kuongeza kiwango cha damu.!

Damu ni sehemu muhimu ya mwili wa binadamu ,damu ina seli za aina tofauti zenye shughuli mbalimbali mwilini. Mojawapo ya seli hizo ni seli nyekundu za damu ambao zina hemoglobin inayoshughulika na usafirishaji wa oksijeni katika mwili wa binadamu.

Upungufu wa hemoglobin hugundulika kwa vipimo vya wingi wa damu hospitalini na mara nyingi upungufu huu humpelekea mtu kupata dalili kama kupata kizunguzungu, kushindwa kupumua vizuri, kupata uchovu na hali ya udhaifu na hata kuumwa kichwa .

Seli nyekundu za damu zinavyoonekana ndani ya mishipa ya damu

Seli nyekundu za damu hutengenezwa na mwili wenyewe kwenye mifupa ya mwanadamu na wingi wake na uzalishaji wake hutegemea hali ya lishe ya mtu na afya yake kiujumla.

Habari njema!!

Habari njema ni kwamba, pamoja na lishe unaweza kuongeza kiwango cha utengenezaji wa seli hizi (na hata kuongeza kiwango cha hemoglobin) kwa kufanya mazoezi.

Mazoezi haya yanayosaidia katika kuongeza kasi ya uzalishaji wa seli hizi huitwa β€œmazoezi ya Aerobic” , haya ni maazoezi yanayohitaji pumzi na hutumia nguvu .Haya ni kama

  • kukimbia,
  • kutembea,
  • kuogelea, na hata
  • kuendesha baiskeli.

Nini hutokea haswa unapofanya haya mazoezi?

Mtu anapofanya mazoezi haya husababisha uzalishaji wa homoni ya ukuaji (Growth hormone) kuongezeka, hivyo kusaidia ukuaji wa mifupa sambasamba hupelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa seli za damu.

Vilevile ,kwa kuwa mwili hutumia kiwango kikubwa cha oksijeni wakati wa mazoezi hii hupelekea mwili kutengeneza seli zaidi ili kufikia lengo la oksijeni itakayotumika.

Kwa kuhitimisha ni vyema kufanya maozezi kwa malengo zaidi ya miili fit ila pia kwa ajili ya afya ya damu zetu ili kuepuka athari za kuwa na damu ndogo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center