Kwanini mishipa ya damu ya mama mjamzito huvimba? (Varicose veins)

Vidonda vya rangi ya bluu hutokea kwenye miguu kwasababu ya mishipa ya damu kuvimba na ni kawaida sana wakati wa ujauzito. Lakini, wakati mwingine mishipa hii huumiza.

Sababu kubwa ya vurugu hii katika mishipa ya damu ya miguuni ni wakati mtoto anakua katika mfuko wa uzazi, kunakuwa na shinikizo kubwa juu ya mishipa ambayo hurudisha damu moyoni kutoka miguuni .Β 

Je, ninawezaje kuepukana na hali hii?

  • Epuka kukaa katika mtindo mmoja kwa muda mrefu.Β 
  • Ikiwa mishipa ya uvimbe iko kwenye miguu, unaweza inua miguu kukaa juu ili kukupa nafuu
  • Fanya mazoezi yatakayosaidia mzunguko wa damu kama vile kutembea.

Mara chache sana, mishipa ya uvimbe inaweza kuendelea mpaka nje ya sehemu ya kijinsia ya mama. Mama huyu anapaswa kumwona daktari au kutembelea kituo cha afya kilichokaribu

Β 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center